Tuesday, September 29, 2015

MANNY PACQUIAO KUDUNDANA NA AMIR KHAN

Manny Pacquiao kurejea ulingoni mwakani, atapigana na nani? jibu lipo hapa…


Bondia wa kimataifa wa Filipino Manny Pacquiao ambaye mwezi May mwaka 2015 alidundwa na bondia mwenye rekodi ya kutopigwa Floyd Mayweather, ameanza kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji katika bega la kulia. Manny Pacquiao mara ya mwisho kuingia ulingoni ilikuwa dhidi ya Floyd Mayweather .
2CE3279F00000578-0-image-a-40_1443517091461
Manny Pacquiao baada ya kushindwa pambano hilo alitoa sababu kuwa moja kati ya vitu vilivyochangia kupoteza pambano hilo ni bega lake ambalo lilikuwa na mauvu, hivyo alipaswa kufanyiwa upasuaji ila ilimlazimu kuingia ulingoni baada ya maandalizi ya pambano hilo, yalikuwa yamekamilika kwa kiwango kikubwa hivyo ilikuwa ngumu kuhairisha.
2CE3279300000578-0-image-a-39_1443517088399
Stori zilizoandikwa jana September 29 ni kuwa bondia huyo atarudi ulingoni mwakani dhidi ya Amir Khan, taarifa hizi zinakuja baada ya Manny Pacquiao kufanyiwa kipimo cha MRI Scan na kugundulika kuwa anaendelea vizuri. Promota wa bondia huyo Bob Arum alithibitisha wiki iliopita kuwa yupo katika mazungumzo na timu ya Amir Khan na mambo yanaenda vizuri.
2CE0076E00000578-0-image-a-37_1443517077500
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment