Mapenzi yanaumiza na wengine wanashindwa kuyahimili maumivu.
Ni
binti Wanjiru Kamanda wa miaka 21 tu ndio amefanya mpaka nimeiandika
hii taarifa hapa, alikua mapenzini na kijana Farid Mohammed (24) lakini
sasa hivi mapenzi yao yamekuwa habari nyingine.Kilichotokea kwa wawili hawa huko Buruburu Kenya ni kwamba msg ya mapenzi ya Mwanamke mwingine ilikutwa kwenye simu ya boyfriend ambaye ni Farid, Wanjiku akashindwa kujizuia na kumchoma kwa kitu chenye ncha kali zaidi ya 20 mgongoni, tumboni, kifuani na kwenye shingo.
Pamoja na Farid kupelekwa Hospitali Madaktari hawakuweza kuokoa maisha yake na kwa sasa Wanjiru amelazwa kwenye Hospitali ya Kenyatta Nairobi Kenya akiwa na pingu kwenye kitanda chake huku Polisi wakiendelea na uchunguzi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment