Bibie hakutaka utani, kaamua kutumia Bango kubwa barabarani kutangaza Ndoa Yake imevunjika..
Kuna msemo wa Kiswahili unasema, ‘Simulia ila usiombee yakukute‘
!! Pata picha tukio la mpenzi wako analipia kabisa liwekwe Bango kubwa
barabarani lenye ujumbe kwamba wewe na yeye biashara yenu imefikia
mwisho, yani hakuna mapenzi tena !!
Watu wa maeneo ya Sheffield, Kaskazini mwa Uingereza wameishuhudia hii yani pembeni ya barabara kubwa kabisa, mwanamke mmoja ambaye jina lake ni Lisa aliona
afanye maamuzi magumu baada ya kutopendezwa na kitendo cha mumewe kuwa
sio mwaminifu kwenye uhusiano wao, mama akaona isiwe shida.. kaenda
kwenye Kampuni ambayo inahusika na kuweka mabango makubwa mjini,
akalipia na yeye litundikwe Bango lenye ujumbe maalum kabisa kwa mumewe.
Jamaa nao kwa sababu hiyo ni biashara
yao hawakuwa na neno, siku ilipofika wakaenda kutundika Bango hilo
ambapo baadhi ya Mashuhuda wamesema walishuhudia Bango hilo
linaning’inia kati ya saa 12 mpaka saa tatu asubuhi, muda ambao kunakuwa
na msongamano mkubwa wa magari kwa wanaowahi kwenye shughuli zao.
Kwenye Bango kulikuwa na maneno ambayo Lisa aliyaandika kwa mumewe Paul kwamba aendelee tu na maisha yake akirudi hatomkuta nyumbani, na anamtakia kazi njema.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment