Monday, September 28, 2015

LOWASA ALITETEMESHA JIJI LA TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, MKUTANO wa mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa, leo  umelazimu kusitisha shughuli zote za biashara na usafirishaji na badala yake watu wengi kwenda katika mkutano wake uliofanyika uwanja wa Tangamano.
Shamrashara za jiji kuzizima zilianza toka asubuhi baada ya vijana wenye pikipiki, magari na kila aina ya vipando vikiwemo magari ya punda na bodaboda za baskeli kupitia mitaani mkuanzia barabara ya kwanza hadi ya 21.
Huduma ya usafiri wa daladala ulikuwa wa kusuasua kuanzia saa 5 asubuhi  baada ya watu wengi kufika katika uwanja wa Tangamano mapema ili kuwahi nafasi na kujionea shamrshamra za mkutano.
Baadhi ya abiria ambao walikuwa wakienda Raskazone na majanimapana wakalazima kushushwa Tangamano badala ya mwisho wa gari kutokana na abiria wote kushuka uwanjani hapo.
Kwa upande wa huduma za maduka wamiliki na wauzaji wakalazima kufunga biashara zao baada ya kukosa wateja kufuatia watu wote kukimbilia Tangamano kusikiliza sera za mgombea Urais wa Ukawa, Edward Lowassa.
Baadhi ya wakazi wa Ngamiani walisema haijawahi kutokea mitaa kuwa meupe na kudhani kuwa hakuna watu na mitaa kukimbiwa ilhali wengi wamenda katika mkutano wa kampeni za mgombea wa Ukawa.
Nao abiria wa bodaboda na baskeli wamevihama vituo vyao kushiriki katika mkutano huo na kuviwacha vitupu na abiria wao kutembea kwa miguu jambo ambalo wengi wamedai imekuwa kero.
“Mimi nimetoka Mikanjuni kwa mguu hadi kufika hapa sijakutana na daladala ya aina yoyote na kila umuonae anelekea uwanja wa mkutano wa mgombea urais wa Ukawa” alisem Mwarami Sharif
Alisema mkutano huo umeleta usumbufu kwa watu wa kipato cha chini ambao hawana usafiri binafsi kwani wengi wao wamelazika kutembea kwa miguu kwenda hospitali kuwaona wagonjwa na wanaorejea majumbani kutoka sehemu za kazi.
                                                   Mwisho
Hata hivyo mkutano huo uliahirishwa kutokana na maelfu ya watu kufurika na kuhatarisha usalama wa watu kutokana na kukosa hewa na kukanyagana na hivyo mgombea huyo wa Urais kusema bora usalama wa wapiga kura wake na hivyo kuwataka siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi na kumuingiza Ikulu.
Taarifa zilizoifikia tangakumekuchablog ni kuwa watu zaidi ya 80 walizimia uwanjani hapo na kupatiwa matibabu katika vituo vya afya iliyosababishwa na kukosa hewa kutokana na wingi wa watu waliojitokeza uwanjani hapo.


 Maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga wakimiminika katika uwanja wa Tangamano kwa kutumia kila aina ya usafiri ukiwemo Punda, Pikipiki Baiskeli na vipando tofauti tofauti ilimradi kufika na kusikiliza sera za Mgombea Urais, Edward Lowassa





 Kutokana na maelfu ya watu kufurika Uwanja wa Tangamano na maelfu wengine walikimbilia katika majengo ya gorofa ili tu kusikiliza na kumuona mgombea Urais , Edward Lowassa ambapo hata hivyo maofisa usalama waliwamuru kushuka ili kuepusha magarofa kuanguka kutokana na wingi wa watu katika majengo hayo





No comments:

Post a Comment