Hawa mastaa nao wamepitia magumu sana, wengine walifungwa mpaka Gerezani..
Maisha ya Mastaa Behind the Scenes
kuna vitu vingi sana huwa nje havijulikani, lakini ukiangalia tu kwamba
wao ni binadamu basi ni lazima kuna time wanakutana na mambo magumu na
wakati mwingine mambo ni poa kama tu inavyotokea kwa mtu mwingine!
Nimeikuta hii story kwenye zile ambazo
zimeandikwa pia kwenye kurasa zinazohusu maisha ya Mastaa mtaani, yani
kwenye maisha yao nje ya sanaa wanazofanya mbele ya Camera.. wengine
story zao zinasikitisha sana ikiwemo kujihusisha na dawa za kulevya,
matukio ya silaha na wapo waliowahi kufungwa pia.
1. Michael Gerard “Mike” Tyson
Mwaka 1991 Mike Tyson alikamatwa kwa kesi ya kubaka, japo mwenyewe alidai kwamba hakufanya kitendo hicho ila iikuwa makubaliano ya wao wawili, yani Mike mwenyewe na Mrembo Young Desiree Washington ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati huo.
Mwaka 1992 alifungwa kifungo cha miaka
sita jela lakini aliachiwa baada ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili,
baadae mwaka 1999 Mike alirudi
tena Jela kutumikia kifungo cha miezi tisa jela baada ya kujeruhi watu
wawili kwenye ajali ya barabarani ambayo aliisababisha.
Mike alikamatwa tena mwaka 2007, alikuwa akiendesha gari huku amelewa, akakaa jela siku moja alafu akafungwa kifungo cha nje kwa miaka mitatu akiwa chini ya uangalizi maalum.
2. Robert Downey Jr
Robert Downey Jr alifundishwa
kutumia Dawa za kulevya na baba yake akiwa na umri wa miaka 8.. kwenye
Kesi alizowahi kukutana nazo iko pia ya kukamatwa akiwa anaendesha gari
kwa speed kubwa huku akiwa na dawa za kulevya, Heroine, Cocaine pamoja
na bunduki. Kuna wakati alilewa dawa za kulevya kiasi cha kujikuta
akipotea na kuingia kwenye nyumba ya jirani yake ambaye alikuwa amelala
wakati wa usiku.
Robert alifungwa
kwa miaka mitatu kifungo cha nje lakini akakiuka masharti ikiwemo la
kutotumia dawa za kulevya, akakamatwa na kufungwa jela miezi sita… jamaa
aliachiwa mwaka 1999 lakini akakamatwa tena baada ya kukiuka sharti la
kwenda kupimwa kama anatumia dawa za kulevya, akakaa Jela mwaka mmoja,
alipoachiwa akaona abadili maisha yake kwa kujiweka busy zaidi na
kucheza movie.
3. Wesley Snipes
Wesley Snipes kuna wakati alijikuta akiingia kwenye Milango ya Magereza na kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kukwepa Kodi.
Jamaa alianza kutumikia kifungo kuanzia mwaka 2000 mpaka 2013, alipotoka akarudi kazini kwa kushiriki kwenye Movie ya The Expendables 3 japo aliendelea kulalamika kwamba mbona wakwepa Kodi wako wengi lakini akakamatwa pekeyake ?!
4. Curtis James Jackson III aka 50 Cent
Kama umepata nafasi ya kucheki movie ya jamaa ya Get Rich or Die Tryin’,
anasema hiyo movie imezungumia sehemu kubwa sana maisha yake kuanzia
alikotoka mpaka alipofika sasahivi, maisha yalikuwa magumu ikafanya awe
karibu sana na matukio ya uhalifu tena wakati akiwa na umri mdogo.
Kama hujui taarifa ikufikie kwamba 50 Cent alianza kuuza Dawa za kulevya akiwa na umri wa miaka 12 tu, 50 Cent aliwahi
kupigwa risasi tisa akiwa kwenye mazingira ya biashara ya Dawa za
kulevya, baadaye mwaka 1994 alikamatwa na Polisi kwa kosa la kukutwa na
cocaine, heroine na Bastola nyumbani kwao…
Alihukumiwa kifungo kati ya miaka mitatu
mpaka tisa jela lakini baadaye aliachiwa huru na kuamua kujihusisha na
biashara safi ikiwemo kuingia kwenye muziki.
5. Ja Rule
Sio stori ngeni kwa marapper wa Marekani
kuingia kwenye matatizo na Sheria za nchi yao… Ja Rule nae amewahi
kujikuta kwenye vitanzi mara kadhaa hivi na kusomewa hukumu kwenda jela.
Ukiachana na ishu ya kukamatwa akiwa na
Bangi na kuendesha gari huku akiwa na leseni iliyokwisha muda wake,
mwaka 2007 aliingia kwenye noma nyingine akiwa na rapper Lil Wayne,
jamaa alikutwa na Bastola pamoja na Dawa za kulevya, akaenda jela miaka
miwili kuanzia mwaka 2010… haukupita muda mrefu akakutwa na hatia ya
kukwepa kodi, akaendelea kutumikia kifungo mpaka mwaka 2013.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment