Sunday, September 27, 2015

ARFICAN SPORTS YAWATOA TONGO WANATANGA

 Kikosi Cha Ndanda FC kilichobugizwa bao 1 na Arfican Sports wana Kimanumanu leo Uwanja wa Mkwakwani Tanga
 Tangakumekuchablog
Timu ya African Sports ya Tanga, imewaondoa aibu wakazi wa Tanga na washabiki wake baada ya kuibamiza bao moja timu ya Ndanda FC ya Mtwara.
Timu hiyo ambayo imeonyesha kandanda safi la ufundi wa hali ya juu tofauti na timu nyengine za Tanga ambazo zimekuwa hazionyeshi ushindani na badala yake zimekuwa zikipokea vipigo mfululizo.
Kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo hadi kipenga cha mwisho African Sports walionyesha kandanda safi na kuwakonga washabiki wake wakiwemo wakazi wa Tanga ambao kipindi cha pili cha mchezo walifanikiwa kutingisha nyavu kwa bao la ufundi.
Baadhi ya washabiki waliofika kuishangilia timu hiyo walizungumza na tangakumekuchablog na kudai kuwa huo ni mwanzo wa safari ya ushindi na kusema kuwa wanatoa salamu kwa timu nyengine ambazo zitakutana nazo.
Walisema katika safari hiyo kwao kila timu inayokutana nayo wataichukulia   sawa na fainal hivyo kuwataka washabiki na wapenzi wa timu hiyo kuishangilia kwa nguvu zote ili kuweza kupata ushindi mfululizo.








No comments:

Post a Comment