Sunday, September 20, 2015

YASIKUPITE MATOKEO YA MAN NA SOUTHAMPTON

Matokeo ya Man Utd vs Southampton nimekuwekea hapa

Ligi kuu ya Uingereza Barclays Premier League imeendelea jioni ya leo kwa michezo miwili kati ya Southampton vs Man United huku Liverpool wakiumana na Norwich.
 
Kutoka katika dimba la St Mary, Manchester United leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Soton ambao wamekuwa wakiisumbua sana United katika miaka ya hivi karibuni.

Mshambuliaji mpya wa United Anthony Martial aliifungia timu yake magoli mawili huku Juan Mata akifunga la tatu – Graziano Pelle aliifungia Southampton magoli mawili.
 
Mechi nyingine ya jioni hii kati ya Liverpool dhidi ya Norwich imeisha kwa sare ya 1-1.

No comments:

Post a Comment