Barcelona watamkosa Lionel Messi leo wakiikaribisha Bayer Leverkusen Uwanja wa Camp Nou
HATUA
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaendelea leo na kesho, huku
mabingwa watetezi, Barcelona wakiikaribisha Bayer 04 Leverkusen Uwanja
wa Camp Nou mjini Barcelona, Hispania.
Katika
mchezo huo, Barcelona watamkosa nyota wake, Lionel Messi aliyeumia
mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las
Palmas Barcelona, lakini hapana shaka Neymar na Luis Suarez watawabeba wababe hao wa Katalunya.
BATE Borisov watakuwa wenyeji waRoma Uwanja wa Borisov Arena, Chelsea wataifuata FC Porto Uwanja wa Dragao, Bayern Munchen wataikaribisha Dinamo Zagreb Uwanja waAllianz Arena, Arsenal wataikaribisha Olympiakos Uwanja wa Emirates, Lyon wataikaribisha Valencia Uwanja waStade de Gerland, Maccabi Tel Avivwataikaribisha Dynamo Kyiv Uwanja wa Bloomfield na Zenit St Petersburg wataikaribisha KAA Gent Uwanja wa Petrovski.
Messi aliumia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las Palmas Barcelona
Michuano hiyo itaendelea kesho FC Astana ikiikaribisha GalatasarayUwanja wa Astana Arena, CSKA Moscow ikiikaribisha PSV Uwanja wa Arena Khimki, Juventus ikiikaribisha Sevilla Uwanja wa Juve, Borussia MonchengladbachikiwakaribishaManchester City Uwanja wa Borussia-Park, Malmo FF ikiwakaribisha Real Madrid Uwanja wa Swedbank, Manchester Unitedikiwakaribisha VfL Wolfsburg Uwanja wa Old Trafford, Atletico de Madridikiwakaribisha Benfica Uwanja wa Vicente Calderon na Shakhtar Donetsk wakiwakaribishaParis Saint-GermainUwanja wa Lviv.
No comments:
Post a Comment