Wednesday, September 30, 2015

MTOTO WA WIKI 5 ASINDWA MASHINDANO YA UREMBO, UINGEREZA

Kutana na mtoto wa wiki 5 tu lakini kavunja rekodi kwenye mashindano ya Urembo..Pichaz


Imezoeleka wanaoshiriki mambo ya urembo ni mabinti  ambao tayari wanajitambua na wenye uwezo wa kujibu maswali pale wanapokuwa wakihojiwa.
Hii imekuwa tofauti kwa Matilda Mackie mtoto aliyeshiriki mashindano hayo akiwa na wiki 5 tu tangu azaliwe huko Uingereza.
Mama wa mtoto huyo Jennifer alipeleka jina la mtoto wake kwa majaji wa shindano hilo la Kitaifa la urembo lililofanyika Glasgow mwezi uliopita na mwanaye kufanikiwa kuhika nafasi ya pili.
Mama huyo amesema nia ya kumshirikisha mwanaye huyo kwenye mashindano makubwa kama hayo ni kuweza kumshinda rafiki yake pamoja na kutimiza ndoto baada ya watoto wake wawili kufanya vizuri.
Amesema anajiona ni mama mwenye bahati kubwa baada ya watoto wake wengine Alexis na Maclan Mackie nao kufanikiwa kushiriki mashindano hayo na kufanya vizuri.

pegant

pgnt2
Matilda Mackie akiwa na mama yake Jennifer

ale
Alexis Mackie

lach
Lachlan Mackie baada ya kushinda

pgnt3
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment