Wednesday, September 23, 2015

BAADA YA HITILAFU, RUBANI ATUA BARABARANI

Pale ambapo mambo hayaendi sawa Rubani anaamua kutua ndege barabarani..

Kuna wakati ambao ikitokea mambo yameharibika angani, Rubani wa ndege anaamua kufanya maamuzi magumu ili kuokoa abiria wake na kuhakikisha hakiharibiki kitu.
Plane
, jamaa walikuwa wanaendesha zao magari kwenye barabara Mitaa ya California, Marekani… wakati wamefika kwenye mataa wakasimama kusubiri kuruhusiwa kuvuka, ghafla ikakatisha ndege ndogo speed kabisa, ikaenda mbele ikasimama !!
airplane-emergency-landing.png.cf
Ripoti ya Polisi haijasema sababu ya ndege hiyo kutua kwenye barabara ya magari, ila ndani ya ndege kulikuwa na Mwalimu pamoja na Wanafunzi wanaojifunza Urubani.. wote walitoka salama na ndege ilitua salama kabisa, hakukuwa na athari yoyote iliyojitokeza japo ni mara chache sana ndege kutua mazingira kama hayo alafu isitokee tatizo.
Unaweza kuplay hizi video kuona hali ilivyokuwa mpaka ndege ikatua barabarani mtu wa nguvu.

Hiki hapa kipande kingine cha video chenye mwendelezo wa tukio hilohilo.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment