Abiria kakosea mlango Ndege ikiwa angani, badala ya chooni akaenda kwenye mlango wa kutokea nje..
Ndege ya Shirika la KLM ilikuwa katikati ya safari kutoka Edinburgh kwenda Amsterdam,
Uholanzi… ilibaki kidogo mambo yaharibike katikati ya safari.. abiria
mmoja akakosea mlango, badala ya kufungua mlango wa kuingia chooni, yeye
akaenda moja kwa moja kwenye mlango wa kutokea nje huku ndege ikiwa juu
angani na safari inaendelea !!
Ingekuwa mlango huo ni mwepesi kuufungua kama mlango wa gari basi mambo yangekuwa tofauti, jamaa huyo James Gray, baada ya ndege kutua Uwanja wa Schiphol Airport alikamatwa
na Askari na kuwekwa ndani kwa saa kadhaa alafu akaachiwa baada ya
kupigwa faini ya Pound 440 ambazo ni kama Tshs. Milioni 1.4.
Adhabu yake haijaishia hapo, jamaa kazuiwa pia kusafiri kwa Ndege za KLM kwa kipindi cha miaka mitano… Kwa vile yeye ni raia wa Scotland,
ilibidi atumie usafiri wa Ndege nyingine kurudi kwao huku akijitetea
kwamba yeye hata hakujua kwamba huo mlango ni wa kutokea nje.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment