Panya wahangaisha ‘jela ya Mandela’
Watu karibu 4,000
wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini baada ya
panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa mmoja.
Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo.Panya hao wameeneza maradhi yajulikanayo kama leptospirosis, yanayosambazwa kupitia mkojo wa wanyama hao waharibifu.
Muungano wa kutetea haki za maafisa wa polisi na maafisa wa magereza umesema gereza hilo lilikuwa limejaa kupindukia..
Mandela alihamishwa kutoka jela ya Robben Island na kupelekwa Pollsmoor mwaka 1982
Maafisa wa afya wanasema hakuna mtu afaaye kurejeshwa kwenye gereza hilo hadi panya wote waangamizwe.
No comments:
Post a Comment