Thursday, September 17, 2015

APIGWA OPERESHENI KUTOA ALMASI TUMBONI

Aliona njia pekee ya kutoroka na jiwe la almasi ni kulimeza… Kilichofuata ni stori nyingine!

Nimekutana na stori kutoka Thailand inayomhuusu mwanamke mmoja kutoka China kukamatwa na alamsi tumboni mwake…
Jiang Xulian ni raia wa China ambaye aljikuta matatani na polisi baada ya yeye na mchumba wake wa Kichina kukiri kuiba jiwe la almasi lenye thamani zaidi ya milion 560 za Kitanzania siku ya Ijumaa baada ya jiwe hilo kuonekana kwenye X-ray scan ya mwanamke huyo.
thai2
Jiwe la almasi lililokuwemo tumboni mwa Jiang.
Jiang na mchumba wake walizuiliwa na polisi kwenye uwanja wa ndege wa Bangkok Suvarnabhumi International Airport walipokuwa wanajaribu kutoroka nchi hiyo… taarifa za almasi hiyo ziliwafikia polisi baada ya mkaguzi wa duka liitwalo ’56th Bangkok Gems & Jewelry Fair’ kutoa ripoti ya kuibiwa kwa jiwe hilo kwenye duka hilo.
>>> “Alipewa dawa za kumsaidia kupata choo lakini siku tatu badaae hakuna kilichotokea, na pale polisi walipojaribu kumpatia chakula aligoma kabisa kula bali alisisitiza apewe maji tu!”<<<  walisema Polisi kituoni hapo.
thai3
Madaktari wakiwa wameshika almasi hiyo waliofanikiwa kuitoa tumboni mwa Jiang!
Baada ya njia zote za Polisi kugoma, kituo cha polisi kilichokuwa kinamshikilia dada huyo kiliamua kufanya utaratibu wa kupata kibali cha hospitali kitakacho waruhusu madaktari  kumfanyia operation mwanamke huyo ili kuitoa alamsi hiyo tumboni mwake… madaktari walifanikiwa, na Jiang anashitakiwa kwa kosa la uwizi na pengine atakuwa matatani kufungwa kwa miaka 3 na faini juu!
thai
Jiwe lenyewe ndio hili hapa, thamani yake mtu wangu inagonga mpaka milion 560 za Tz… ndio mtu alikuwa anajaribu kutoraka nalo!
Issue kama hii unaambiwa ishawahi kutokea mwaka 2012 huko South Africa pia baada ya polisi kumkamata mwanaume aliyekuwa anajaribu kutoroka nchini humo na alamasi zaidi ya 220 tumboni mwake! Nae kama Jiang alikamatwa uwanja wa ndege baada ya X-ray scan kunasa alamasi hizo tumboni mwake!
  Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment