Bidhaa za China zimekuwa na umaarufu
mkubwa sana kwenye nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo, lakini sababu
kubwa ni kwamba ukiangalia Takwimu za mwaka 2013 na 2014 China imetajwa
kuongoza kwa kuwa Nchi yenye Viwanda vingi zaidi Duniani… kwa kuanzia
hapo tu kuna uhalali pia China kuongoza kwa kuzalisha baadhi ya bidhaa.
Hongera nyingi kwao, Ripoti hii hapa
nimekutana nayo, kumbe kuna bidhaa ambazo China imetajwa kuongoza kwa
kuziingiza bidhaa hizo sokoni sehemu mbalimbali Duniani !! Usishangae
pia kuna bidhaa ambazo nusu ya zile zinazotumika Duniani zimetoka China,
japo wengine wanalalamika kwamba bidhaa za Kichina ni FEKI !!
China
inazalisha 70% ya simu zimu zote zinazotengenezwa Duniani, hiyo ni mara
kumi zaidi ya wastani wa simu zinazotengenezwa kwenye nchi nyingine
Duniani.
Ripoti zinaonesha China
imetengeneza Computer Milioni 286 kwa mwaka 2014, unaambiwa idadi hiyo
inakaribia 91% ya Computer zote zilizotengenezwa Duniani mwaka 2014.
Wastani wa Idadi ya viatu vinavyozalishwa China kwa mwaka ni Bilioni 13, hiyo ni kama 63% ya viatu vyote vinavyotengenezwa kwa mwaka Duniani.
China wako vizuri mtu wangu, kwenye Air Conditioners
zinazozalishwa Duniani, wao wametengeneza kama 80% hivi ya zote. Kwa
hesabu nyingine ni unaambiwa jumla ya AC Bilioni 109 zinatengenezwa
China kwa mwaka.
Viwanda vingi viko China, ndio… na hata vya Meli vipo huko pia mtu wangu, kwenye idadi ya Meli zinazotengengezwa kila mwaka Duniani, China wana wastani wa kuzalisha Meli Milioni 766, hiyo inagusa kama 45% ya Meli zote zinazozalishwa Duniani kila mwaka.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment