Tangakumekuchablog
Tanga, WAKULIMA
wa kilimo cha mahindi Tanga, wametakiwa
kuunda vikundi vitakavyopelekea kupeana
taarifa za kupatikana masoko ili kuepuka kulanguliwa na watu wenye pesa.
Akizungumza katika warsha ya siku
moja ya Wadau wa Mnyororo wa thamani wa mahindi
iliyoitishwa na BRAC, jana kupitia Mradi wa kuziwezesha Kaya Masikini Vijijini (LEAD) , Msimamizi wa kilimo Tanga na Morogoro, Gwakisa Albon, alisema
wakulima wengi wa kilimo wamekuwa
hawaendelei kwa kutojua upatikanaji wa masoko.
Alisema hali hiyo imekuwa chanzo cha
kutokuwa na soko la uhakika jambo ambalo linapelekea kulanguliwa mazao yao na
hivyo kuwa chanzo cha kuwa watumwa wa matajiri.
“Hapa tupo na wakulima wa mahindi na
wauzaji wa pembejeo za kilimo pamoja na wadau wa kilimo----tunatambua kuwa
wakulima wengi hawaendelei kutokana na kutokuwa na umoja” alisema Albon na
kuongeza
“Nawaomba nyinyi wakulima hebu
undeni vikundi ambavyo mutaweza kupeana taarifa za masoko na kilimo----kuwa
mbalimbali kunapelekea kuwa masikini na mtaji wa matajiri” alisema
Kwa upande wake, Mkulima wa kijiji
cha Pongwe Gedion Chagonja ametaka Serikali kupunguza gharama za pembejeo ili
kuweza kulima kilimo cha ksasa chenye tija ikiwa na pamoja na kuwakopesha
wakulima.
Alisema wakulima wengi wanashindwa
kuendeleza kilimo chao kutokana na gharama kubwa za pembejeo za kilimo na hivyo kulima kilimo cha mazoea jambo ambalo
linarudisha nyuma nguvu kazi katika sekta ya kilimo.
“Tunaiomba Serikali kupunguza
pembejeo zakilimo pamoja na kutukopesha kwani sisi wakulima wadogo wadogo tuko katika wakati mgumu wa kuendeleza kilimo
chetu” alisema Chagonja
Chagonja pia ameishauri Serikali
kupanga bei moja ya pembejeo za kilimo na kuondokana na mfumo wa sasa wa bei
tofauti jambo ambalo limekuwa likiwachanganya wakulima.
Alisema bei kuwa tofauti imekuwa
ikiwapa kero wakulima hao na hivyo kuitaka Serikali kuingia kati mfumuko wa bei
za kiholela ili kuwa wezesha wakulima kulima kilimo cha ksiasa na kuondokana na
nkilimo cha mazoea.
Mwisho
Washiriki wa Warsha ya Wadau wa Mnyororo wa Thamani wa Mahindi Tanga wakiwa katika mafunzo ya namna ya kulima kilimo chenye tija iliyoandaliwa na BRAC kupitia mradi wa kuenua kaya masikini vijijini (LEAD) warsha iliyofanyika Tanga jana.
Afisa Masoko Mradi wa BRAC Kupitia Mradi wa kuenua kaya masikini vijijini (LEAD) akitoa somo la namna ambavyo wakulima wanaweza kuendesha kilimo chao kwa faida ikiwa na pamoja na kuunda vikundi pamoja na kuyafikia masoko.
No comments:
Post a Comment