Wednesday, September 16, 2015

FULL TIME YA SIMBA NA MGAMBO, MATOKEO YAKO HAPA

 

MPIRA UMEKWISHAAAAA
DK 90+2
SUB Dk 86 Simba wanamtoa Ndemla anaingia Nd'aw
 Dk 85, Kessy anaingia na mpira, anapiga krosi safi lakini kipa anaokoa vizuri


Dk 75 hadi 80 mpira unachezwa katikati zaidi kwa kila upande 
GOOOOO Dk 73, Kiiza anafunga bao kwa shuti kali baada ya mabeki wa Mgambo kuzubaa kuondosha hatari

Dk 72, krosi safi kabisa lakini Kiiza anapiga kichwa ‘mtoto’ na kipa anaudaka
SUB DK 67 Mgosi anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajib

DK 57 HADI 61, mpira unaonekana kuchezwa katikati zaidi lakini Mgambo wanaonekana kuwa vizuri zaidi

Dk 55, krosi nzuri ya Tshabalala inamkuta Majabvi lakini anaukosa mpira

Dk 51, Kiiza anapiga vizuri kabisa, mpira unagonga mtambaa wa panya na kurudi uwanjani

Dk 47, Kessy anapiga krosi safi lakini lakini Mgosi anakuwa mfupi na kushindwa kuuwahi
SUB Dk 46 Simba wanamtoa Kazimoto anaingia Kiiza


Dk 46, Mgambo wanafanikiwa kuutumbukiza mpira wavuni, lakini kabla aliyepiga alikuwa ameotea

MAPUMZIKO
DK 43-45 Mechi inaonekana kupoa na timu kucheza zaidi katikati ya uwanja

Dk 40, Simba wanaonekana kuimarika lakini mashabulizi yao mengi hayana macho.
Dk 32, Mgosi anaingia vizuri lakini Mwalyanzi anaangushwa. Faulo Simba wanapita kuipokea

GOOOOOO Dk 27 Majabvi anaifungia Simba bao safi baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Tshabalala aliyepewa pasi fupi kutoka kwenye kona na Mwalyanzi.


Dk 26 Simba wanafanya shambulizi kali, Kessy anapiga shuti linaokolewa, Mgosi naye anapiga shuti kali linaokolewa pia na kuwa kona

Dk 25, Mgosi anageuka nje ya eneo la 18 na kupiga shuti la chini lakini linaokolewa na kipa

Dk 23, Simba wanapasiana vizuri, Majabvi anajaribu kupiga shuti lakini linakuwa kuuuubwaaa kama mnazi!

Dk 19 Maganga tena anapiga shuti kali lakini Manyika anaokoa
Dk 17, Salim Gilla anapiga shuti kali kwa mpira wa faulo lakini Manyika anaudaka vizuri kabisa

Dk 15, pasi nzuri ya Mgosi, Kazimoto anapiga shuti kali lakini kipa anadaka kwa ulaini kabisa

Dk 9 Maganga anaingia vizuri lakini kabla ya kupata nafasi nzuri ya kupiga shuti, Tshabalala anaondoa hatari

Dk 6, Mgosi anapiga shuti la chini linagonga mwamba na kurudi uwanjani. Mgosi alipata pasi nzuri kutoka kwa Mwalyanzi.

Dk 5, Simba wanafanya shambulizi jingine, krosi safi ya Ndemla inamfikia Mgosi lakini mwamuzi anasema ameotea.

Dk 3 Tshabalala anachonga kona nyingine lakini Mgambo wanaokoa tena.

Dk 2, Ndemla anaingiza krosi safi lakini inaokolewa na kuwa kona. Tshabalala anachonga kona safi inaokolewa na kuwa kona ya pili.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment