Sunday, September 20, 2015

JOSE MOURINHO NA MIPANGO YAKE

Mechi sita, kashinda mechi mbili, kafungwa tatu na sare moja, mipango ya Mourinho ipo hapa..

Baada ya kuanza vibaya kwa Ligi Kuu Uingereza kwa upande wa klabu ya Chelsea, kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho inaripotiwa kuanza mipango mbadala ya kuimarisha kikosi chake, Chelsea ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Uingereza, hadi sasa imecheza mechi sita, imeshinda 2, sare 1 na kufungwa 3.
img_620_142405
Ruben Neves
Stori kutoka dailystar ni kuwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameanza harakati za usajili kuelekea dirisha dogo, inaripotiwa Jose Mourinho ametenga kiasi cha pound milioni 20 ili kuimarisha safu yake ya kiungo kutokana na kuanza vibaya msimu huu.
marko-grujic
Marko Grujic
Mourinho ana mpango wa kuimarisha safu yake ya kiungo na inatajwa kufuatilia nyendo za Ruben Neves kutokea FC Porto na Marko Grujic kutokea Red Star Belgrade. Paul Pogba wa Juventus yupo katika mipango ya Mourinho ila ushindani kutoka kwa FC Barcelona kumtaka nyota huyo, kunamfanya mkenye Victor Wanyama kupewa nafasi kubwa ya kujiunga na Chelsea.
Victor Wanyama mwenye umri wa miaka 24 amebakiza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Southampton, hivyo inaonyesha yuko tayari kuvunja mkataba wake na kujiunga na klabu nyingine, kwani awali kabla ya dirisha la usajili kufungwa aliomba klabu yake imuuze kwenda Tottenham Hotspur.
55fdb53012925_GettyImages483098894
Victor Wanyama
Kingine kinachoongeza uwezekano wa Chelsea kumsajili ni kuwa, Wanyama wanaweza kumtumia katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani klabu yake haishiriki. Wanyama alijiunga na Southampton mwaka 2013 kwa ada ya pound milioni 12.5 dau lililoweka rekodi ya usajili kwa mchezaji kutoka klabu za Scotland kwenda Uingereza.
Kwa habari, matkuio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment