Tangakumekuchablog
Tanga, ALIEKUWA MKUU wa
Mkoa wa Tanga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalulla, ameiagiza bodi ya Usajili wa Wabinu Majengo
na Wakadiriaji Majenzi, kuwachukulia hatua kali za kisheria wabadhrifu na wala
rushwa ndani ya bodi hiyo.
Akifungua kongamano la 24 ya bodi ya
Usajili Mkoani hapa leo, Magalula, alisema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa
wakivunja maadili ya kazi zao ikiwemo kujihusisha la ulaji rushwa jambo ambalo
limekuwa likirudisha nyuma bodi hiyo.
Alisema ili kuweza kupiga hatua za
kuwaletea maendeleo wananchi ni vyema bodi ya Usajili ikifanya ukaguzi mikataba
ya makampuni kwa madai kuwa huko ndiko ubadhrifu unakoanzia.
“Jambo la faraja ni kuona wenyeviti
wakuu wa taasisi na watendaji mbalimbali muko kwa pamoja hapa na hiki ambacho
mutakijadili na kuadhimia kitakuwa cha faida kwa maslahi ya maendeleo ya
wananchi” alisema Mgalula na kuongeza
“Ila jambo la msingi naiagiza bodi
ya usajili wa ubunifu majengo kusafisha wala rushwa kila idara-----jambo hili
limekuwa likirudisha nyuma jitihada za bodi” alisema
Alisema wala rushwa wamejificha kila
idara na hivyo kuitaka bodi hiyo kufichua makucha yake kwa kuwafichua na
kuwaweka hadharani ikiwa na pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Akizungumza katika kongamano hilo,
Msajili wa bodi, Abdalla Jihad, alisema bodi hiyo imewachukulia hatua za
kisheria wataalamu waliokiuka taaluma zao 92 na makampuni 57 yamefutiwa usajili
kwa kukiuka sheria.
Alisema hatua hizo imesaidia kwa
baadhi ya wataalamu kuzingatia maadili na nafasi zao ikiwa na pamoja na
makampuni kuzingatia sheria za usajili jambo ambalo imekuwa msaada kwa bodi.
“Katika kusimamia sheria bodi
imeweza kuwachukulia hatua za kisheria wataalamu tisini na mbili sambamba na
makapuni 57 yaliyokiuka sheria” alisema Jihad
Alisema kwa mantiki hiyo bodi
imejipanga kuhakikisha wataalamu wanazitumia nafasi zao na kuziba mianya yote
ya rushwa na ubadhrifu wa pesa ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea.
Mwisho
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment