Hii ndio miji ya Africa inayokadiriwa kuja kuwa na mamilionea wengi kufikia mwaka 2020!
Dunia inabadilika sana siku hizi mtu wangu, watu na wawekezaji wengi sana wanaitupia jicho Africa wakiamini hii ndio sehemu pekee iliyobaki yenye uwezo wa kuikomboa dunia ya kesho.
Nimekutana na stori moja kwenye mtandao inayosema kufikia mwaka 2020 Africa itakuwa ni miongoni mwa sehemu zitakazokuwa na ongezeko kubwa la Mamilionea wa Kiafrica, hii ni kutokana na utafiti uliofanyika na kuonyesha kama ukuaji wa uchumi na shughuli za kibiashara zikiendelea kukua kutakuwa hakuna haja wa Mamilionea wa Africa kuwekeza pesa zao sehemu nyingine.
Kati ya miji iliyotajwa kuwa na vigezo hivi ni mji wa Lagos wa Nigeria, Accra wa Ghana, Johannesburg wa South Africa na Dar es salaam wa Tanzania.
Kufikia mwaka 2012 Dar Es Salaam ilikuwa na idadi ya mamilionea 1,900 na makadirio yanaonyesha kutokana na ukuaji wa uchumi wetu wa Tanzania kufikia mwaka 2020 jiji la Dar es salaam litakuwa na idadi ya mamilionea wasiopungua 3,000!
Licha ya miji hii 4 kuwa yenye vigezo vikubwa zaidi nchi zingine za Africa zenye mamilionea wengi ni; mji wa Cairo uliopo Egypt, Cape Town uliopo South Africa, Kano ulipo Nigeria na Marrakesh uliopo Morroco.
Picha hii hapa chini inaonyesha makadirio ya ongezeko mamilionea Africa kufikia mwaka 2020 kwenye miji mingine ya Africa…
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment