Wednesday, September 2, 2015

SOMA HABARI KUBWA ZILZIOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, SEPT 02 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha elimu cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, Kituo pia kinatoa kozi mbalimbali za kielimu na kiufundi ukiwemo wa Umeme na Computer, Kituo kipo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
NIPASHE
Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limemshikilia na kumhoji kwa zaidi ya saa tano mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa chama hicho, Anthony Komu , kwa madai ya kumtisha kwa bastola Katibu wa chama hicho mkoani hapa, Basil Lema.
Hata hivyo, baada ya kuhojiwa jeshi hilo lilimwachia huru Komu na kisha kulifuta jalada la uchunguzi lililofunguliwa dhidi yake baada ya mlalamikaji (Lema) kuomba shauri hilo limalizwe katika meza ya usuluhishi ndani ya Chadema.
Komu alisema alishikiliwa na kuhojiwa kuanzia saa 5:00 asubuhi na kuachiwa saa 10:00 jioni.
Niliwaeleza kwamba sijawahi kumiliki silaha na sina mpango wa kuimiliki wakaridhika na maelezo yangu na wakakubali mzozo uliotufikisha hapo tukaumalize nje ya vyombo vya sheria,” alisema.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, alithibitisha kwamba mgombea huyo wa ubunge Jimbo la Moshi Vijijini kupitia Chadema alikuwa alitumiwa ujumbe wa kuitwa polisi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hiyo.
Agosti 18, mwaka huu wakati wa marudio ya uchaguzi wa kura ya maoni za Chadema katika jimbo hilo, Komu akiwa katika eneo la Kibosho, Moshi Vijijini alidaiwa kumtisha kwa bastola katibu huyo wa mkoa alipomfuata akitaka kujua taratibu zilizotumika kuhamisha mkutano wa uchaguzi huo ambao ulipangwa kufanyika katika eneo la Garden, kata ya Kiboroloni, Manispaa ya Moshi.
Naye Lema akizungumzia suala hilo alisema: “Ni kweli tumemalizana na bosi wangu (Komu) baada ya kuafikiana wenyewe na kuomba polisi ikubali mambo haya yamalizwe nje ya vyombo vya kisheria kutokana na maslahi mapana ya Chadema.”
NIPASHE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema asilimia kubwa ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu yamekamilika, huku karatasi za kupigia kura zikitokea Afrika Kusini.
Aidha, tume hiyo imesema gharama  za awali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama vile wino, fulana, kofia, karatasi za kura, vibanda vya kupigia kura na vifaa vya kufungashia katika uchaguzi huo hadi sasa zimefikia Sh. bilioni 31.25.
Imesema dola za Marekani 6, 145, 882.92 sawa na Sh. bilioni 13.1 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ununuzi karatasi hizo za kura. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Manunuzi na Menejimenti ya Lojistiki wa Nec, Eliud Njaila, wakati akizungumza Dar es Salaam jana.
Alisema karatasi hizo zinatarajia kuanza kuwasili nchini Septemba 29 hadi Oktoba 15, mwaka huu.
Alisema gharama za vifaa hivyo ni tofauti na zile zilizotumiwa na tume hiyo kwa ajili ya kununulia  mashine 8,000 za Biometric Voters Registration (BVR) na shughuli nzima ya uandikishaji kwenye Daftari la Wapigakura nchi nzima, ambazo kwa mujibu wa Nec ni Sh. bilioni  133.
Tume hiyo pia ilisema Sh. bilioni 85 zilitumika kulipa posho waandikishaji, wataalamu wa mashine hizo, kutengeneza kadi, karatasi, wino na vifaa muhimu wakati wa uandikishji kwenye daftari hilo nchini kote.
Alitaja kampuni iliyoshinda zabuni ya wazi ya kutengeneza karatasi hizo kuwa ni Uniprint ya nchini Afrika Kusini ambayo alisema ina uzoefu mkubwa katika kazi hiyo kwani ndiyo iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vifaa hivyo katika uchaguzi mkuu  nchini humo  wa  Tanzania wa mwaka 2005.
 NIPASHE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepokea rufaa 54 za madiwani kupinga maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini.
Taarifa ya Nec iliyotolewa jana, ilieleza kupokea pia jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali.
“Tume imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na wagombea (warufani) na wasimamizi wa uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge,” taarifa hiyo ilieleza na kuongeza:
 “Leo (juzi) zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa 38. Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya tume na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia maamuzi ya kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi.”
Iliongeza kuwa wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi ni 16 na Tume imerudisha wagombea 13 kati ya hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi.
“Hii ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha makosa ya kisheria au kiufundi,” iliongeza taarifa hiyo.
NIPASHE
Sakata la madeni ya walimu limezidi kuchukua sura mpya baada ya serikali kusema haidaiwi na kwamba imebaini kuwapo kwa majina hewa ya walimu zaidi 4,000 yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo.
Imesema imegundua hivyo baada ya kufanya uhakiki wa deni la Sh. bilioni 19.6 lililowasilishwa na walimu baada ya kuwalipa madai yao kwa mara ya mwisho mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, baada ya kuhakiki madeni hayo mwaka jana, serikali imegundua deni halisi inalodaiwa na walimu ni  Sh bilioni 5.6 tu.
Alisema endapo serikali isingefanya uhakiki wa deni hilo na kulilipa ingeingia hasara ya Sh. bilioni 14.
Alisema katika uhakiki huo, wizara hiyo imebaini kulikuwa na deni hewa kubwa la mwalimu mmoja wa Halmashauri ya Tunduru Mkoani Lindi Sh. milioni 500 na kwamba baada ya kuhakiki imegundua deni lake halali ni Sh. 500,000 tu.
Dk. Likwelile alisema kwa madeni ya mwaka jana, serikali imelipa walimu Sh. bilioni 5.6 baada ya kufanya uhakiki.
“Katika uhakiki tumebaini kuwapo udanganyifu wa fedha kwa walimu kujiongezea huku wengine wakidai deni la aina moja mara nne,” alisema.
Dk. Likwelile alitaja sababu za serikali kukataa kulipa baadhi ya madai ya walimu yaliyowasilishwa ni pamoja na kukosa vibali au vielelezo, madai mengine kuwa yameshalipwa, mishahara iliyowasilishwa kama madai yasiyo ya mishahara, baadhi ya walimu kutotambuliwa na halmashauri, baadhi ya walimu kutokuwa na madai katika majalada na makosa ya ukokotoaji na uandishi.
JAMBOLEO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepokea rufaa 54 za madiwani kupinga maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini.
Taarifa ya Nec iliyotolewa jana, ilieleza kupokea pia jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali.
“Tume imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na wagombea (warufani) na wasimamizi wa uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge,” taarifa hiyo ilieleza na kuongeza:
“Leo zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa 38. Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya tume na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia maamuzi ya kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi.”
Iliongeza kuwa wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi ni 16 na Tume imerudisha wagombea 13 kati ya hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi.
“Hii ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha makosa ya kisheria au kiufundi,” iliongeza taarifa hiyo.
MTANZANIA
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema endapo atachaguliwa kuongoza Serikali ya awamu ya tano, atahakikisha anashusha bei ya saruji na mabati ili kila Mtanzania aweze kufurahia maisha kwa kujenga nyumba bora na nzuri.
Amesema hatakuwa tayari kuona bei ya vifaa vya ujenzi ikipaa hali ya kuwa viwanda vipya vitaanza uzalishaji.
Kauli hiyo aliitoa jana katika mikutano yake ya kampeni za kuomba kuchaguliwa kuwa rais katika wilaya za Namtumbo,
Tunduru mkoani Ruvuma na Masasi mkoani Mtwara, ambapo alisema amejipanga kuwatumikia Watanzania kwa dhati kwa kuleta mageuzi ya kiuchumi.
“Kuanzia mwaka kesho tutashusha bei ya saruji na mabati ili kumwezesha kila Mtanzania popote alipo aweze kujenga nyumba bora. “
“Na sasa muda mfupi ujao kitaanza uzalishaji na sisi Mkoa wa Ruvuma tujiandae kwa kupokea mapinduzi ya maendeleo na kiuchumi bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini na hata ukabila,”
Akizungumzia kuhusu uhusiano, alisema Serikali yake itaendelea kuimarisha uhusiano na nchi zote jirani kama ilivyokuwa katika awamu zilizopita.
Dk. Magufuli alisema katika kuhakikisha nchi inaendelea, itakuwa karibu na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
Alisema anaomba achaguliwe yeye ndio mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania pamoja na nchi za Ulaya.
“Nichagueni mimi naaminika na nchi zote, msichague mtu asiyeaminika mbele ya wahisani, kama mtachagua mtu wa aina hiyo wahisani wanaweza wasiendelee kutoa misaada.
“Nilikuja hapa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara na Rais Kikwete, na sasa kazi inaendelea na
ujenzi.
“Lengo la Serikali ya CCM ni kuiunganisha nchi kwa mtandao wa barabara, na sasa Jaica wapo wametupatia fedha kwa ajili ya ujenzi Namtumbo hadi Mtambaswala mkoani Mtwara,”.
Akizungumzia madini ya uranium yalipo wilayani Namtumbo, alisema Serikali yake itayaendeleza ili yaweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi.
Akiwa njia kuelekea Tunduru, Dk. Magufuli, alijivua kwa muda kofia ya ugombea na kulazimika kurejea katika nafasi yake ya Waziri wa Ujenzi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara katika Kijiji cha Uliya.

 MTANZANIA
Baadhi ya viongozi wa dini na wananchi wamesema shutuma za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kuwa baadhi yao walihongwa na Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, ni upuuzi mtupu.
Wamemtaka atoe ushahidi wa madai hayo kwa kutaja majina ya viongozi na kiasi walichohongwa, wakisisitiza kuwa hizo ni siasa za majitaka na kwamba anaifanyia kazi CCM ili apate njia ya kurudi katika chama hicho.
Rais wa TEC azungumza
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amemtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi wa madai yake kuwa maaskofu wa kanisa hilo wamehongwa na Edward Lowassa.
Askofu Niwemugizi alieleza kushangazwa na tuhuma hizo zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya maaskofu bila uthibitisho.
“Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote.
Askofu Niwemugizi alimtaka Dk. Slaa kutoa uthibitisho wa maaskofu wa kanisa hilo kupokea fedha kutoka kwa Lowassa waweze kutoa uamuzi.
“Lowassa nimewahi kukutana naye nilimwalika kwenye shule yangu ya seminari kule Biharamulo… shule yenyewe inaitwa Katoke na nilimuweka wazi sababu za kumwalika na sikupokea kiasi chochote cha fedha kutoka kwake,”alisema askofu huyona kuongeza
“Athibitishe hilo aonyeshe kiasi cha fedha na majina ya maaskofu, mimi sijapata kiasi chochote labda kama nimetupiwa kwenye akaunti yangu bila mimi kujua lakini nasisitiza atoe ushahidi.”
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekosti, William Mwamalanga alisema kauli za Dk. Slaa zina dalili ya kuleta kisasi fulani.
“Angekuja mapema kabla ya taratibu hizi kuanza tungemwelewa lakini kwa sasa yupo nyuma ya wakati. Kwanza ameonekana amesukumwa afanye aliyofanya na hilo haliwezi kuwabadilisha Watanzania walioamua kutaka mabadiliko,”alisema na kuongeza: “Hotuba yake haina mashiko na taifa halihitaji watu wabinafsi,”alisema Mchungaji Mwamalanga.
Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kuwa mshenga wa Edward Lowassa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) .
Pia amekana kuhusika kuwarubuni kwa fedha maaskofu 30 wa Kanisa Katoliki ambao wanadaiwa kumuunga mkono Lowassa katika mbio zake za urais baada ya kuhongwa fedha.
Askofu Gwajima alisema Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyokuwa imebakia ndani kati ya bunduki ya CCM ili kuwaokoa.
Alisema yote yaliyosemwa na Dk. Slaa ni tuhuma za uongo hivyo wananchi wazipuuze kwa kuwa mwanasiasa huyo anatafuta uungwaji mkono kwa wananchi aelekee CCM.
“Yaani ni uongo kabisa tena uongo mweupe, imedhihirisha wazi kuwa huyu mtu asingefaa kuwa rais. Ni dhahiri ameona akiwasema wanasiasa wenzake watamjibu kwenye majukwaa yao ya siasa, lakini sasa amewasema maaskofu kwa kuwa wao hawana majukwaa.
“Kwa hiyo namshauri hayo mambo ya kuwahusisha maaskofu na uchaguzi aache uongo wa namna hiyo. Nafikiri awaseme wanasiasa wenzake kuzungumzia mambo ya siasa ila kuwahusisha maaskofu si mambo ya busara,” alisema.
Akizungumzia suala la kuwa mshenga wa Lowassa na Chadema, Askofu huyo alisema anafikiri Dk. Slaa ametumwa na waliomtuma, hivyo anawafanyia kazi watu.
“Kwa kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana, inatakiwa awepo mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti maana, haiingii akilini… ameingiza Gwajima, Rostam (Aziz) na maaskofu, haeleweki anachozungumza. Lakini ninachosema kuna waliomtuma ni watu ambao anawafanyia kazi.
“Kikubwa ni kwamba baada ya Lowasaa kuchaguliwa kugombea urais kwa Chadema alichukia, alifikiri Lowassa hataendelea kuwa na umaarufu, sasa anaona Lowassa anakwenda, hiyo imemtia hasira anataka kumchafulia Lowassa, ndiyo maana anaongelea Lowassa Lowassa tu.
“Kwa mfano alisema Lowasa angekuja na wabunge wenyeviti wa CCM, ina maana angemkubali Lowassa aje nao, sasa angekuja nao asingekuwa fisadi? Ni swali zuri ila amekwepa kulijibu.
“Nafikiri Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyobakia ndani ya bunduki ya CCM. Natoa wito kwa waumini wangu wafahamu kuwa hizi tuhuma ni za uongo na namsihi huyo daktari asihusishe maaskofu na uongo wake abaki nao mwenyewe,” alisema Askofu Gwajima.
HABARILEO
Baada ya kutoweka hadharani tangu Julai 28, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani na kuelezea kilichomsibu, akiweka wazi kwamba amestaafu siasa baada ya chama hicho kumpokea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye amesisitiza hawezi kukwepa kashfa ya Richmond.
Alisema Lowassa si kiongozi anayefaa kuwa rais wa nchi kutokana na kuhusika na vitendo vya rushwa na kwamba ni mhusika namba moja katika kashfa ya Richmond, iliyomwondoa madarakani Februari 2008.
Tangu Julai 28, wakati Lowassa alipoanza kuonekana katika vikao vya Chadema, Dk Slaa amekuwa haonekani katika vikao vya chama hicho ikiwemo Mkutano Mkuu uliomtangaza Lowassa kuwa mgombea urais wa chama hicho na umoja wa wapinzani (Ukawa) katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Mbali ya Mkutano Mkuu, Dk Slaa hakuonekana katika matukio muhimu kama yale ya Lowassa kufika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya kugombea urais na wakati wa kuirejesha, na pia katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwenye Viwanja vya Jangwani, Agosti 29, mwaka huu.
Katika mkutano wa jana, Dk Slaa alieleza kwa kirefu kilichotokea na kumfanya kupotea katika harakati za Chadema huku akiweka wazi kuwa ujio wa Lowassa ulimfanya ajiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu, tofauti na madai ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kwamba alikuwa likizo. “Nimejitokeza leo, mimi sikuwa likizo
Mengi yamesemwa na viongozi wangu, lakini ukweli ni kwamba sikupewa likizo na yeyote, nasisitiza sina barua yoyote ya likizo.
“Kilichotokea ni kwamba niliamua kuachana na siasa tangu tarehe 28/7 majira ya saa 3 usiku, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama changu na sikukubaliana nayo,” alisema Dk Slaa na kuongeza: “Wapo watu wanaosema Dk Slaa alishiriki kutoka mwanzo katika ujio wa Lowassa.
Nilishiriki kweli, lakini niliweka msingi tangu dakika ya kwanza kutaka kujua Lowassa anakuja Chadema kama mali au anakuja kama mzigo? Msimamo wangu huu haukupatiwa majibu na hadi sasa viongozi wa Chadema hawana majibu katika hili.”
Akisimulia mkasa mzima, padri huyo wa zamani wa Kanisa Katoliki alisema baada ya Lowassa kukatwa kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM mjini Dodoma, alipigiwa simu na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aliyemwita kuwa mshenga wa Lowassa, akimuarifu hatua hiyo ya kukatwa Lowassa ni mtaji kwa Chadema.
Alisema katika maelekezo yake, Askofu Gwajima alimuelekeza Dk Slaa awasiliane na Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe kuhusu mpango huo na kumrejeshea majibu ya kile walichoafikiana na kwamba alitekeleza ombi hilo kwa kuwasiliana na Mbowe na baadaye walimkaribisha Askofu Gwajima ili kuzungumza kwa kina.
“Tangu wakati huo niliweka msimamo wangu. Unajua kwa kawaida ni vizuri kumsikia mtu ana nini na si kutomsikiliza kabisa. Chadema ni chama cha siasa haikatazwi kumpokea mtu.
“Niliweka msimamo kwanza atangaze kutoka ndani ya CCM, baada ya kutangaza hilo atangaze pia ni chama gani anakwenda, halafu tatu atumie nafasi hiyo kujisafisha na tuhuma zake anazoshutumiwa.

MWANANCHI
Mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa amesema akiwa rais wa Awamu ya Tano atafuta maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini waliodumu tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961.
Lowassa aliyekuwa akitumia staili ya kuwauliza wananchi matatizo yanayowakibili na kisha kuwajibu atakavyoyatatua, alisema tangu nchi ipate uhuru maisha ya Watanzania ni duni na kuahidi kuwaondoa katika umasikini.
Wakati Lowassa akisema hayo, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye aliwataka wananchi kuipa Chadema na Ukawa miaka mitano tu ili iweze kuwaletea maedeleo na kama wakishindwa, warudi tena CCM.
“Jambo kubwa ni kupiga kura na kuzilinda na ikiwezekana akina mama mpike chakula kabisa nyumbani ili waume zenu wakifika nyumbani wajipakulie wenyewe.
Tusipoitoa CCM madarakani hatutaweza kuwatoa tena na lazima wang’oke safari hii. Hata wanaCCM wenzangu nawashauri waondoke huko na kujiunga na sisi.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na watu wachache ikilinganishwa na mikutano mingine ya kampeni ya mgombea huyo wananchi hao walieleza kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa maji na umeme, migogoro ya ardhi, ada na michango iliyokithiri katika shule pamoja na ushuru katika mazao.
“Tutamaliza tatizo la umeme ndani ya mwaka mmoja, tutamaliza suala la kuporwa ardhi,” alisema Lowassa huku akiwahoji wananchi wa kijiji hicho kwanini wakubali kuporwa ardhi.
Wananchi hao walisema katika vituo vya afya wagonjwa wanaruhusiwa kurudi majumbani kutokana na vituo hivyo kukosa maji sambamba na kutozwa ushuru wa mazao usiokuwa na kichwa wala miguu.
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye alisema maendeleo ya Tanzania hayafanani na rasilimali zilizopo nchini, akiwataka wananchi kuyakubali mabadiliko ili kuepuka matatizo mengine.
“Nilikuwa waziri mkuu kwa miaka 10 lakini nchi haikuwa na vita. Mkichagua upinzani kutakuwa na amani kama kawaida,” alisema Sumaye huku akitolea mfano yaliyotokea Masasi ambapo wananchi walichoma moto vituo vya polisi na Halmashauri baada ya bodaboda kugongana na gari la polisi, “Hali hiyo inatokana na wananchi kuchoka
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment