Wachina na njia mpya za kulipa bili za vyakula…
Najua kuna wale watu wangu wanaopenda
kutoka kila weekend kula good time na watu wao huku wakipiga stori mbili
tatu.. lakini ikifika wakati wa kulipa watu wanakimbia bili na usipokaa
vizuri utajikuta bili ya watu wote unalipa wewe.
Wachina
wameona hili ni tatizo kwa vijana wengi sana ambao labda kwa namna moja
ama nyingine wanalazimika kuonyesha kiasi cha pesa wanachochangia pale
bili inapokuja mezani na pengine kuona aibu kuhofia labda wakichangia
pesa ndogo watachekwa, hivyo wameamua kuleta kitu kinachoitwa ‘WeChat Communication Tool’.
Hii ikoje? WeChat Communication Tool ni application ya kuchat kama vile ilivyo Whatsapp lakini
tofauti ni kwamba kwa kutumia application hii unaweza kulipia bili ya
chakula kwa kupiga picha kile unachotaka kuchangia kulipa na kuituma
kwenye ‘WeChat Wallet’ na kumaliza kila kitu huko bila kutoa pesa yako mfukoni!
Zaidi ya watu million 600 China
wanatumia hii application sio tu kwa kulipia chakula bali hata kwa
huduma nyingine ndogondogo kupitia simu zao za mikononi, lakini huduma
ya ulipaji wa bili za vyakula kwa kuchangia kupitia WeChat Wallet ilianza rasmi mwaka jana na toka kipindi hicho idadi ya watumiaji wamekuwa wakiongezeka kila siku.Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment