Serikali
ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya
kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Rais
huyo alitakiwa kukamatwa kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu madai ya uhalifu wa
kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe.
Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa Bara la Afrika na kwamba Serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
Lakini gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka katiba.
Katika taarifa ,Serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini humo.
Mahakama kuu imeipatia Serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment