Monday, June 29, 2015

JIJI LA NANJIANG LAKUMBWA NA MAFURIKO

Kama ulidhani  mafuriko ni Tanzania pekeake, angalia picha 10 kilichotokea China..

d43d7e14d47316fadabd07
May 2015 ulikuwa mwezi ambao tulishuhudia maafa yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha mfululizo Dar… mara nyingi hivi vitu vikitokea huku kwetu watu hawaamini kama hata nje ya TZ nako huwa vitu vinatokea hivyohivo.
Mafuriko yametokea China, hapa unaweza kuona kwenye picha hali ilivyokuwa baada ya balaa la mafuriko kuwakuta.
d43d7e14d47316faf2e232
Hivi ndio ilivyokuwa kwenye Chuo kilichopo Nanjing, Jimbo la Jiangsu ndani ya China… Watu zaidi ya 65,000 wameathirika kutokana na mvua hizo.
d43d7e14d47316fada8506
Hii ni sehemu ya familia zilizoathiriwa na mafuriko, hapo wamepata hifadhi ya muda Dingyan Primary School, iliyopo Jiji la Changzhou China.
d43d7e14d47316fadb0408
Familia nyingine zilizopata hifadhi katika Shule ya Msingi. Watu wamelazimika kulala madarasani
d43d7e14d47316fadb1409
Bibi mwenye umri wa miaka 70 akitokwa machozi baada ya kuokolewa kwenye nyumba iliyokumbwa na mafuriko.
d43d7e14d47316fadbb00b
Hawa jamaa nao wako kwenye harakati za kujiokoa
d43d7e14d47316fadbc00c
Mwonekano wa mtaani nyumba zimefurika maji
d43d7e14d47316fadbd20d
Kikosi cha Waokoaji wakiwa wamembeba mmoja ya watu toka kwenye nyumba zilizofurika maji
d43d7e14d47316fadbe10e
Nao wamepumzika baada ya kupata hifadhi kwenye Shule ya Msingi.
7427ea210c5416faf2a952
Hali ilivyo kwenye mitaa mingine katika Jiji la Sichuan, China.
Pichaz zote zimepigwa jana JUNE 28 2015.
Kwa habari, matukio, michezo na burudani, ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment