Thursday, June 25, 2015

AFRIKA KUSINI YATISHIA KUJIONDOA ICC

Afrika Kusini huenda ikajiondoa kwenye ICC

null
Afrika Kusini imesema kuwa huenda ikajiondoa kutoka  Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi kufuatia jaribio la kumkamata rais wa Sudan Omar al Bashir alipokuwa nchini humo.
Hata hivyo  kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Lakini baada ya kikao maalum cha Baraza la Mawaziri nchini humo, Serikali ilitoa onyo kuwa huenda ikalazimika kujiondoa kutoka kwa makubaliano yeyote na mahakama ya ICC kutokana na sababu kadha.
Mahakama ya Afrika Kusini ilikuwa imemualika Rais Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo la kukamatwa kwake..
Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake Rais Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurejea nyumbani.
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba Serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa ni mwanachama wa ICC.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado zipo.
Rais al Bashir anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
Kwa habari, amtukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment