Wednesday, June 24, 2015

WATU 18 WAUWAWA XIJIANG, CHINA

Watu 18 waaga dunia Xinjiang UChina

Ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa watu 18 wameaga dunia katika eneo la Uchina la Xinjiang katika makabiliano na polisi katika eneo la ukaguzi.
Radio Free Asia inasema kuwa watu hao wa kabila la Uighurs walitumia visu na mabomu kuwashambulia maafisa wa polisi.
Hakujakuwa na mawasiliano rasmi kuhusu tukio hilo lakini wafanyikazi wa hospitali katika mji wa Kashgar wameiambia BBC kuwa maafisa hao wa polisi walipokea wahanga wa tukio hilo.
Moja ya lengo huenda ni kuweka vikwazo vikali kwa waislamu wa Uighurs katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan. Chanzo BBC
Kwa habari , matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment