Saturday, June 20, 2015

MAUAJI YAZUA MJADALA MAREKANI

Mauaji yazua mjadala wa ubaguzi US

Matumizi ya neno ''uhalifu wa chuki'' ili kuelezea mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la watu weusi mjini Carolina Kusini nchini Marekani umezua mjadala kuhusu ni nini haswa kinachosababisha mtu kutekeleza ugaidi.
Watu wengi wameonyesha hasira zao kuhusu  afisa mkuu wa polisi mjini Charleston alivyoelezea kisa hicho wakati wa mkutano na vyombo vya habari.null
Wanasema kuwa ''uhalifu wa kivita'' sio neno zito linalofaa kutumika kuelezea kisa hicho na kudai kwamba iwapo waathiriwa wangekuwa watu weupe na mshukiwa kuwa mwenye asili ya Asia,ama mweusi neno ugaidi lingetumika.
Mshukiwa Dylan Roof , mwenye umri wa miaka 21 ameshtumiwa kwa kuingia ndani ya kanisa saa tatu za usiku siku ya jumatano na kuwapiga risasi waumini waliokuwa katika maombi.
 
null
Katika picha ya mtandao wake wa facebook mshukiwa huyo alikuwa amevalia jaketi lililo na picha na bendera ya Rhodesia na Afrika kusini.
Kanisa la Kiafrika la kimethodisti lina historia ndefu kama eneo la vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na ni muhimu katika historia ya Wamarekani weusi.
 
null
Mwanaharakati Martin Luther King na Coretta Scott wote walizungumza katika eneo hilo.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment