Wednesday, June 24, 2015

KILA MTANZANIA KULIPA SHILINGI 100

Kila mwananchi Tanzania anatakiwa achangie shilingi 100/=, unajua ni kwa ajili ya nini?

strategy (1)
Kwenye headlines toka Dodoma labda hii ilikupita, Wabunge wamesikika mara nyingi wakilalamika kwamba Serikali itafanya maisha yawe magumu baada ya kutangazwa kwamba bei ya mafuta itabidi ipande ili kuchangia miradi ya usambazaji wa umeme TZ.
Uchumi wako utategemea mchango wako unaoutoa katika Taifa hili… Tukiona wafadhili wanatusaidia ni kwa sababu wanachukua Kodi ya mwananchi wa kule wanakuja kutusaidia. Kama tuna uchungu wa nchi hii ni lazima mwananchi achangie shilingi mia moja yake ili tumpelekee umeme kule aliko“>>> Saada Mkuya.
Hatuwezi kupitisha bakuli kwa wafadhili tukaomba fedha ili tupeleke umeme vijijini.. Kama tunataka maendeleo ya kiuchumi ya Mwananchi hii tozo tumeipendekeza tunaomba Wabunge mtusapoti kwenye hili
Ni lazima mwananchi achangie maendeleo ya nchi yake.. Tunaomba shilingi mia kwa kila ya mafuta ya taa, petroli na diesel kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini… Hesabu zetu zimeonesha katika tozo hii tutapata shilingi Bilioni 276.. Tukitegemea fedha za wafadhili katika kutekeleza miradi ya maji inawezekana tusifike tunakotaka kufika”>>> Saada Mkuya.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment