Mama mjamzito akatumia pombe aliyoyapata pamoja na mtoto atakayezaliwa…
Wapo wanawake ambao ni wajawazito na wanatumia vilevi, Mbunge Kidawa Hamid Salehe akauliza swali kuhusu athari za vilevi kwa mtoto aliye tumboni.
Naibu Waziri Steven Kebwe akatoa haya majibu >>> “Dawa
za kulevya na vileo vikali zina madhara kwenye mfumo wa mwili wa
binadamu ikiwemo mtoto ambaye hajazaliwa… Madhara yanayoweza kujitokeza
kwa motto ni pamoja na kupunguza ukuaji wa Ubongo, kuathirika kwa mfumo
wa uzazi pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa Ubongo, kuharibika kwa
mimba sambamba na kuzaa watoto njiti…
Mtoto
akizaliwa uwezo wa kujifunza unakuwa mdogo, anakuwa na tabia ya
kutotulia mahali pamoja, kuwa na wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo nap
engine motto akafia tumboni.
Kuna uwezekano pia mama akaambukizwa magonjwa ya zinaa, au kusababisha mtoto kuzaliwa na ngozi kama ya mzee”>>> Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment