Ebola yaibuka mjini Freetown
Maofisa
wa afya nchini Sierra Leone wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili wapya
wanaougua ugonjwa wa ebola na kwamba wamegunduliwa katika mji mkuu wa
nchi hiyo Freetown.
Hapo awali ilidhaniwa kwamba mji huo ulikuwa
hauna maambukizi ya ugonjwa huo,na hakukuwa na wagonjwa walioripotiwa
hapo kabla kwa muda wa wiki kadhaa.Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwa sababu vituo vyote vya karantini vitAendea kazi yake baada ya kufungwa mjini Freetown.
Kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.
Nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment