Tuesday, June 30, 2015

MUGABE AMKEBEHI, OBAMA

Maneno ya utani ya Rais Mugabe kwa Obama baada ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja…

mugabe
Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu Ndoa za jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.
Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
obama
Rais wa Marekani Barack Obama
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na Rais Barack Obama.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni  wafuasi wa shetani wanaoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment