Ripoti nyingine ya idadi ya watu wanaotumia dawa za kulevya China !!
Headlines nyingi sana kuhusu China na
ishu ya dawa za kulevya… Tumeshasikia nyingi kuhusu Sheria zao kali,
zimeshasikika stori za watu waliokamatwa, wengine wananyongwa… leo kiko
kingine kilichoripotiwa huko na hapa tayari kimenifikia.
Moja ya stori kubwa kwenye headlines leo
inahusu ishu ya ongezeko la watu wanaotumia dawa za kulevya… Stori
hiyo imeyafungua mengine kwamba kumbe mwaka 2014 idadi ya watumiaji wa
dawa za kulevya iliongezeka ambapo watu 46,300 waliingia kwenye list ya
watu wanaotumia dawa hizo China.
Ripoti ya China National Narcotics Control Commission ambao wanahusika na udhibiti wa dawa hizo, inaonesha wengi wao ni vijana ambao umri wao ni chini ya miaka 35.
Kwa sababu China wamejitahidi sana kuzuia dawa za kulevya kama Cocaine na Heroine
kuingia ndani ya nchi yao, unaambiwa sehemu kubwa watu hao wanatumia
dawa ambazo ni kemikali pamoja na vidonge na watumiaji wenyewe
ni watu zaidi ya Milioni 1.4
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment