Mama na mtoto wake walivyopona kwenye ajali ya ndege Colombia.. (Pichaz)
Kuna ajali ikitokea alafu unaambiwa wapo
watu waliotoka wazima, inakuwa stori ya kushtua watu wengi sana, tena
ajali yenyewe unaambiwa ni ya ndege!
Ndege bado ni usafiri salama duniani
lakini ajali zake huwa mbaya pia, na ni mara chache kukuta imetokea
ajali alafu wapo waliopona.. ajali ya ndege imetokea Jimbo la Choco,
Colombia siku tano zilizopita, leo ishu iliyo kwenye headlines inahusu
mama mmoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja ambao
walikuwemo ndani ya ndege iliyopata ajali na wametoka hai!
Mama wa mtoto huyo Maria Nelly Murillo amekutwa akiwa na majeraha madogomadogo pamoja na alama za kuungua, lakini mtoto amekutwa salama kabisa!
Wahusika wa Kitengo cha kuongozea ndege
wanasema ndege ilipata ajali baada ya kupoteza mawasiliano kama kwa
dakika 20 hivi, walianza kuitafuta na baada ya siku mbili wakakuta
mabaki ya ndege kwenye msitu mkubwa… kupona kwao ni kama bahati tu,
haijawekwa idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye ndege ila rubani Carlos Mario Ceballos nae alikutwa amefariki.
Maria amesema baada ya ajali alifanikiwa
kufungua mlango wa ndege na kukimbilia kwenye msitu wakati huo ndege
ilianza kuwaka moto tayari.. ndani ya ndege kulikuwa na samaki pamoja na
nazi, mwanamke huyo aliweza kuishi siku zote hizo kwa kunywa maji ya
nazi pekeyake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment