Wednesday, June 24, 2015

CHINA HAKUNA MCHEZO ISHU YA MADAWA KULEVYA

Headlines nyingine ni China na dawa za kulevya, hawana utani kwenye hii ishu !!


cHINA IIIJana niliipata record nyingine kubwa toka China, ishu ni wao na dawa za kulevya… Kwenye ripoti hiyo nikayajua mambo matatu; kwanza ni kwamba kuna ongezeko la watu 46,300 ambao wanatumia dawa za kulevya.
China II
Nyingine ni kwamba kumbe idadi ya watu wanaotumia dawa za kulevya imefikia watu Milioni 1.4 ndani ya nchi hiyo, alafu kumbe dawa wanazotumia ni kemikali na vidonge ambavyo vimatengenezwa kwa matumizi mengine tu, wao wanatumia kama dawa za kulevya !!
China
Leo imenifikia nyingine, Jimbo la Guizhou China jana hiyohiyo wameteketeza dawa za kulevya ambazo zina uzito wa kilo 1,200.. Hiyo imefanyika siku tatu baada ya Maazimisho ya siku ya Kupambana na dawa za kulevya China.
China wako serious kabisa kwenye mapambano na dawa za kulevya, ukikamatwa nazo ni ishu.. na wakizikamata hawaziachii pia !
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment