Malkia kuhama kasri la Buckingham
Shughuli za ukarabati zitagharimu pauni milioni 150 za Uingereza.
Mojawapo ya mapendekezo ya jamii ya kifahari ni kuwa, kasri hilo linahitaji kuwekwa upya mifereji ya kupitishia maji pamoja na maji taka, nyaya zote za umeme zinafaa kutolewa na kuwekwa mpya na pia mapambo hayajafanyika tangu mwaka 1952.
Haya yanajiri baada ya kampuni ya Crown Estate, ambayo inamiliki rasilimali kwa niaba ya malkia, iliporejesha faida ya pauni milioni 285 fedha ya walipa ushuru mwaka jana na kufikisha kiwango hadi asilimia 6 nukta 7.
Ufadhili wa malkia unatarajiwa kupanda kwa pauni milioni mbili mwaka ujao na kufikia pauni milioni 42 nukta 8.
Mwaka jana, malkia alipata pauni milioni 37 nukta 9 kutoka katika hazina hiyo ambapo alitumia pauni milioni 35 nukta 5.
Kiwango hicho kitapanda na kufikia pauni milioni 40 nukta 05 mwaka huu.Chanzo BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment