Saturday, June 20, 2015

JENGO LA GOROFA 57 LAJENGWA KWA SIKU 19 TU

Wachina na balaa zao yani, utakubali kuishi ndani ya ghorofa lililojengwa kwa siku 19 tu?

mini-sky-city-chinaKama unaishi kwenye nyumba yako kabisa labda nianze na hili swali, nyumba yako umeijenga kwa muda gani mpaka imekamilika? Au kama unajenga unatarajia nyumba yako itakamilika kwa muda gani? Kama unahitaji ujenzi wa mjengo wako ukamilike haraka basi unaweza kumpa hilo dili Engineer huyu wa Kichina!!
Zhang Yue amekamilisha kazi ya Ujenzi wa Jengo la Ghorofa lililopewa jina la Mini Sky City  ndani ya China, Jengo hilo lina urefu wa Ghorofa 57 na kazi yote imekamilika kwa muda wa siku 19 tu !!Sky City
Wachina hawana utani, kazi ilipigwa mchana na usiku…  Zhang alivyosimamia huo ujenzi wake ulioiweka China kwenye headline nyingine !!

Vipi ikitokea unatakiwa kuishi ndani ya mjengo huo utakua na amani mtu wangu?
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekucha blog

No comments:

Post a Comment