Wednesday, June 24, 2015

BABA AMFANYIA KITU KIBAYA MTOTO WAKE

Baba analalamikiwa kufanya ukatili kwa mtoto wake kisa homework…

sad
Mara nyingi tumezoea kuona ukatili kwa watoto ukifanywa na wakina mama lakini pia kuna baadhi ya wababa wanatabia ya kunyanyasa watoto wao waliowazaa wenyewe.
 leo inatokea Msasani, Dar es saalam baada ya baba kumwadhibu kwa kumchapa na waya kwenye makalio na kumsababishia majeraha makubwa sana mtoto wake mwenye umri wa miaka 10 kwa kosa la kutofanya homework.
Mtoto huyo alisema siku ya tukio alitumwa na baba yake kwenda kununua mihogo na aliporudi alimkuta baba yake anakagua madaftari na kumuuliza kwanini hajafanya homework, pamoja na kujitetea baba huyo alichukua waya na kumchapa kwenye makalio kisha kumfungia ndani hadi majirani walipokuja kumwokoa.
Hata hivyo kwa sasa baba huyo ameshikiliwa na polisi katika kituo cha Osterbay huku mtoto huyo akichukuliwa na viongozi wa dawati la jinsia hadi hapo sheria itakapochukua mkondo wake kutokana na kutomfahamu mama yake, na mama alipotafutwa alisema aliamua kutoroka baada ya kuchoka kipigo kutoka kwa mume wake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment