Monday, June 22, 2015

BRAZIL YATINGA ROBO , COPA AMERIKA

Brazil yaingia robo fainali Copa America

Thiago Silva na Roberto Firmino walifunga bao moja kila mmoja na kuisaidia Brazil kujikatia nafasi ya kuingia katika robo fainali ya mchuano ya Copa America baada ya kuilambisha sakafu Venezuela.
Silva alifunga kona maridadi baada ya kupata pasi kutoka kwa Robinho huku akianza mechi hiyo kwa nafasi ya Neymar baada ya kupigwa marufuku katika michuano hiyo.
Awali Firmino alibabatiza krosi ya Miku na kufunga bao la kufutia machozi.
Sasa Brazil itamenyana  na Paraguay katika mchuano wa robo fainali mnamo siku ya Jumamosi.
Colombia na Peru pia zilifuzu baada ya kutoka sare tasa mapema mchana.
Katika michuano mingine ya robo fainali, Chile itavaana na Uruguay Ijumaa, Juni 25, Bolivia wavaane na Peru, huku Argentina wakikwaruzana na Colombia,
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment