Utafiti:Watoto waongo ni werevu
Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto
wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na
wale wasiodanganya.
Watafiti katika chuo kikuu cha Sheffield kwa
siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya
mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma yao.Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.
Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo.
Kwa habri matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment