Real Madrid wametoa uamuzi kuhusu kumuuza Sergio Ramos Man United
Saa zisizopungua 48 baada ya klabu ya Manchester United kuripotiwa kutuma ofa ya kumsajili beki wa kimataifa wa Spain, Sergio Ramos, klabu yake ya Real Madrid imepokea ofa hiyo na imetoa uamuzi.Manchester United, juzi walituma ofa ya £35million kwa ajili ya kupata saini ya Ramos na klabu ya Madrid wameipiga chini ofa hiyo.
Madrid walimpa taarifa Ramos juu ya uamuzi wao wakati CEO wa klabu hiyo Jose Angel Sanchez alipokutana na Ramos na wawakilishi wake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Ramos, 29, aliondoka kwenda mapumzikoni huku akiiambia klabu kwamba anataka kufahamu hatma yake kwenye kikosi cha Madrid kabla timu haijakutana kwa ajili ya kwenda kwenye Pre Season Tour mnamo July 10.
Real, pia, hawataki kumpa mwanzo mgumu kocha wao mpya Rafael Benitez kutokana na mgogoro huu wa Ramos.
Ramos amekasirishwa sana baada ya kuona hapewi thamani anayostahili na ameonyesha kuwa tayari kwenda Old Trafford.
Inafahamika kwamba Ramos anapokea mshahara £4m kwa mwaka ndani ya Bernabeu na anataka kupewa mkataba mpya utakaokuwa na thamani ya £6.5m. United wanatajwa kuwa tayari kumtimizia matakwa yake ya mshahara kwa kumpa ofa ya ya mshahara wa £7.8m ili ahamie Old Trafford.
Baada ya Madrid kukataa ofa hiyo sasa taarifa zinasema klabu hiyo inaandaa ofa mpya na itatumwa hivi karibuni.
Ofa hiyo haitomuhusisha golikipa David De Gea kwa namna yoyote.
No comments:
Post a Comment