Saturday, June 27, 2015

SERIKALI YA KENYA YAONYESHA NJIA , KULINDA UTAMADUNI NA UTU WA WAKENYA

TV za Kenya marufuku kuonyesha  video ya ‘Singida Dodoma’

Dodoma Singida 2Mzaliwa wa Tanzania Colonel Mustafa ni msanii wa siku nyingi kwenye muziki Kenya alikokulia na kutengeneza nyimbo nyingi zikiwemo ‘hey baby’ ft. Marya na Mtaani.com ft. Avril ambapo this time yuko kwenye headlines na  video yake mpya ya Dodoma Singida.
Kwenye Interview na mtandao wa kijamii unaofanya vizuri wa milardayo Mustafa amethibitisha kwamba video yake mpya imefungiwa kuonyeshwa kwenye vituo vya TV kutokana na warembo walioonekana ndani yake, yani kutokana na mavazi waliyovaa na kujiachia.
Mustafa amesema hajajutia uamuzi wa kuifanya hiyo video na sio kitu kibaya kwake, mbona za kina Nicki Minaj zilizowazi kuliko hizi zinapigwa na vituo hivyohivyo vya TV Kenya? hii inakuwa sio video ya kwanza kutangazwa kutoonyeshwa kwenye TV,

No comments:

Post a Comment