Tuesday, June 23, 2015

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Kila mama mjamzito na chaguo lake la chakula, lakini mama huyu starehe yake ni Stori nyingine!!

pregna
Inafahamika kuwa wanawake wengi wanapopitia kipindi cha ujauzito wanapata mabadiliko mbalimbali ikiwemo kuchagua aina ya vyakula vya kula pamoja na mambo mengine ambayo ni tofauti na wanapokuwa katika hali ya kawaida.
Jess Gayford ambaye ni mjamzito anatambua kuwa watu wengi watakuwa wakishangazwa na hatua ya yeye kula miche ya sabauni na pia kunywa sabuni za maji lakini ukweli ni kwamba ladha ya sabani kwake imekuwa ni nzuri na kumfanya ajisikie furaha kula.
prenga2
Jess Gayford akiwa na mchumba wake Lee Trimby,
Anasema kama ilivyo kwa watu wengine kutotambua ladha ya sabuni, naye aliitambua baada ya kupata ujauzito wake wa pili ambao kwa sasa una miezi nane.
Jess raia wa Uingereza anasema pamoja na tabia yake hiyo lakini madaktari wamesema hatakua na madhara yoyote kwake wala kwa kiumbe aliyeko tumboni na angalau sasa amepunguza na anakunywa sabuni za maji zilizopo kwenye chupa za milimita 350 mbili kwa wiki na mche mmoja wa sabuni kwa siku.
Kwa habari, matukio, michezo pamoja na vituko ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment