Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
NIPASHE
Serikali imeondoa Muswada wa Sheria ya
Haki ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 Bungeni huku ikiahidi kwamba
Muswada huo utasomwa katika Bunge la kwanza la Serikali ijayo.
Akitoa taarifa ya kuondolewa kwa Muswada huo Waziri Prof. Mark Mwandosya alisema Muswada huo
“Serikali
imetafakari maoni ya kamati na kuafiki muswada uendelee kufanyiwa kazi
hadi hapo kamati itakapokamilisha kazi yake ipasavyo na kuwakilisha
maoni yake Bungeni,“alisema Prof. Mark Mwandosya.
Juni 22 2015, wadau mbalimbali wa habari
waliokutana Dar kupinga muswada huo, kwa kile kinachoelezwa kuwa
unakiuka Sheria za Kimataifa, Katiba ya nchi na unawanyima haki raia
kupata taarifa.
NIPASHE
Jitihada za Mbunge Andrew Chenge
kutaka asihojiwe na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma
‘zimekwaa kisiki’ baada ya shauri la pingamizi lake alilofungua
Mahakama Kuu kutupwa.
Chenge
ni miongoni mwa watumishi wa Umma waliotajwa katika kashfa ya mgawo wa
fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW zilizotolewa na mfanyabiashara James Rugemalira.
Februari 25, mwaka huu Chenge baada
ya kusomewa mashtaka tisa na baraza kabla ya kuhojiwa aliwasilisha
pingamizi la amri ya Mahakama linalodai kuzuia Mamlaka zozote kujadili
au kufanya kazi ya suala lolote la ESCROW.
Siku iliyofuatia Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu Hamisi Msumi alitupilia mbali pingamizi hilo na kueleza kuwa Baraza lina haki ya kumhoji Chenge,
lakini hakukubaliana na uamuzi huo na kusema anakata rufaa Mahakama Kuu
kuomba mwongozo wa Mahakama kuhusu kuendelea kujadiliwa suala hilo au
la.
Jana Jopo la Majaji wa Mahakama hiyo jijini Dar es Salaam, Gadi Mjema, Fauthi Twaibu na Rose Teemba walisikiliza mapingamizi yaliyowekwa na Chenge
na washtakiwa Juni 1 na 2, mwaka huu, na maamuzi yakatolewa kwamba kesi
hiyo imetupiliwa mbali Baraza hilo lina uwezo wa kuendelea na shauri
dhidi ya Chenge.
“Nimetendewa haki, huo ndio uamuzi wa Mahakama nimeridhika nao sina la kusema,” alisema Chenge huku akicheka.
Ofisa Habari wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Johanither Barongo amesema wamepata taarifa za maamuzi ya Mahakama na watatoa taarifa zaidi Jumatatu.
MWANANCHI
Jana ilikuwa siku ya aina yake kwa msanii Faiza Ally na mzazi mwenzake, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Wakati Faiza
akimwaga chozi katika chumba cha habari katika gazeti la Mwananchi
alipofika kutoa ujumbe wa kuomba radhi kutokana na vazi la kitenge lenye
kambakamba alilovaa siku ya KTMA 2015, Sugu alimwaga chozi bungeni
Dodoma alipowataka wabunge wasijadili mambo yake ya faragha.
Faiza
akiwa amevaa baibui na kufunika kichwa kwa hijabu, alieleza kwamba
anajutia kutokana na kuvaa vazi lililoonyesha sehemu kubwa ya makalio
yake alilodhani ulikuwa ubunifu.
“Siwezi
kurudia kosa, nitakuwa makini zaidi katika mavazi yangu, Wasanii wengi
ni wabunifu na hufanya mambo kwa nia ya kufurahisha mashabiki kama
ambavyo amekuwa akifanya Joti kuvaa nguo za kike na kupaka rangi ya
mdomo, hivyo mavazi yangu yalikuwa na lengo la kutoka tofauti mbele za
mashabiki wangu, lakini kwa yaliyonikuta hasa kwenye vazi la Kili
niliomba msamaha kwa jamii na bado naomba wanisamehe”, alisema Faiza Ally akiwa kwenye Ofisi za Gazeti la Mwananchi huku akitokwa machozi.
Mbunge Sugu aliongea
Bungeni kwa uzito akieleza suala lote; “Kwa taarifa tu pamoja na
Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni
mstaarabu, nimetoa nafasi ili majadiliano ya kifamilia yafanyike. Naomba
mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa,” alisema Sugu ambaye alionekana
akifuta machozi akisikitishwa suala hilo kuzua mjadala bungeni.
MWANANCHI
Prof. Mark Mwandosya ambaye anawania kuteuliwa na CCM kugombea urais amemtaka Edward Lowassa kujiunga
na kambi yake kwa kuwa makada wengine wanne kwenye mbio hizo wanamuunga
mkono japo wawili kati ya makada hao wanne wamekana kumuunga mkono.
Mwandosya aliwataja Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Steven Wasira, Samuel Sitta na Bernard Membe kwamba wanamuunga mkono na hivyo kumshauri Lowassa kujiunga na kambi yake.
“Kama
wengi wananiunga mkono, aliyebakia basi atakuwa ni ndugu yangu, rafiki
yangu, Edward Lowassa. Naye angesema hivyo ingerahisisha sana kazi ya
Chama, ingepunguza sana kazi, makundi yangekuwa yameisha,” alisema Mwandosya baada ya kurejesha fomu za kuomba CCM impitishe kugombea urais.
Prof. Mwandosya
alisema mchakato huo umewafanya wanaoomba Urais kuwa marafiki zaidi
licha ya kupigana vijembe, huku akisema ingekuwa nchi nyingine
wangefanyiana vurugu.
“Namshukuru
Benard Membe ambaye ametangaza kwamba yeye ameona katika orodha yote
ya watu 40, kama si yeye basi ataniunga mkono.. Mheshimiwa Pinda,
amelizungumzia hili katika vituo kama si kimoja viwili kuwa moyo wake
utakuwa na furaha kama Profesa Mwandosya anaweza kuteuliwa na chama”—Prof. Mwandosya.
HABARI LEO
Mbunge David Kafulila amemwandikia barua Spika Anne Makinda kumwomba aitake Serikali iwasilishe hoja juu ya sakata la mabehewa feki ya Shirika la Reli Tanzania ili ijadiliwe na Wabunge.
“Kwa
kuzingatia taarifa iliyotolewa na Mamlaka inayosimamia Udhibiti na
Manunuzi , ununuzi wa mabehewa uliofanywa na Kampuni ya India ulikuwa na
mapungufu… kwa sababu Waziri wa Uchukuzi alikiri kupokea Ripoti hiyo,
tunaomba iletwe Bungeni”—David Kafulila.
Katika barua hiyo Mbunge huyo alisema
mapungufu mengine ilikuwa ni Kampuni hiyo kulipwa pesa kabla
haijayafikisha Mabehewa hapa nchini.
Kafulila alisema sakata hilo linahusisha sh. Bilioni 230 na halipaswi kukaliwa kimya.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment