Saturday, June 20, 2015

MAHAKAMA AUSTRALIA YAZUIA MAMA KUNYONYESHA KUTOKANA NA TOTOO MWILINI

Tattoo inaweza kuzuia usinyonyeshe mtoto? Nna hii story toka Australia

Breastfeeding
Michoro ya mwilini aka tattoo ni urembo mwingine kwa watu wengi hasa vijana… Mama mmoja Australia ana mtoto mchanga lakini hatoweza kumnyonyesha mtoto wake kutokana na agizo la Mahakama !!
Vipimo vya Hospitali havijaonesha kama mama huyo ana tatizo lolote, ila ishu ni tattoo ambayo alijichora, Mahakama ilipokea malalamiko kutoka wa mume wa mwanamke huyo kuhusu tattoo aliyojichora kwenye kidole na mguuni.. wakamzuia asimnyonyeshe tena mtoto huyo kutokana na kanuni zilizowekwa na Australian Breastfeeding Association.
Bado kuna mvutano kwenye ishu ya uamuzi huo, CEO wa Australian Breastfeeding Association, Rebecca Naylor yeye anapingana na uamuzi huo wa Mahakama.

Kwa habari matukio na michezao ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment