Wednesday, June 24, 2015

WANYAMA KUTOROSHWA IMERUDI TENA BUNGENI

Kuna watu hawajaisahau ishu ya wanyama kutoroshwa Tanzania, hii imetoka Bungeni Dodoma jana June 23 2015


GiraffeIshu ya wanyama kutoroshwa TZ iliingia kwenye headlines na kusababisha baadhi ya Mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri ikiwemo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kusimamishwa kazi… hii ishu wapo walioisahau na wapo ambao hawajaisahau kabisa.
Imerudi tena ndani ya Kikao cha Bunge leo June 23 2015 >>> “Wakati tunamuwajibisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Ezekiel Maige kwas sakata la utoroshaji wa Wanyamapori, Wizara ilisema itaunda Tume ya Uchunguzi kwenda Qatar kuchunguza na Tume hii iliunda, nataka kujua kwa nini Tume hii isiende Qatar na mpaka sasa Serikali imekaa kimya“>>> Christowaja Mtinda.
Serikali kukiri tukio hili kutokea kwenye Uwanja wa Ndege na inakuja na mkakati wa kuimarisha Ulinzi katika Viwanja vya ndege, wakati wanyama wanatoroshwa ina maana Viwanja vya Ndege havikuwa na Ulinzi?”>>> Christowaja Mtinda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akaja na majibu haya >>> “Kuna tatizo limetokea, kukiri ni uungwana lakini kuna hatua tumechukua kuhakikisha tatizo halitokei tena ikiwemo kufukuza wahusika wote
Iliundwa Tume, tulifanya Uchunguzi na kazi inaendelea, kwa mujibu wa Sheria kwenda kwenye nchi nyingine ni mpaka tupate kibali kwa hiyo tunashughulikia kupata kibali kwenda Qatar”>>> Mohamed Mgimwa.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment