Tuesday, June 23, 2015

SURUALI ZA KUBANA ZALETA KIZAA ZAA AUSTRALIA

Unapenda suruali za kubana?? Haya ndio yaliyomkuta mwanamke mmoja Australia !!

skinny-jeans-for-women
Kama wewe ni mtu wa fashion na style za kisasa kwenye ishu ya mavazi, basi hii stori iwe karibu na wewe mtu wangu… Kuna fashion ya watu kuvaa nguo za kubana, umeipata stori ya Australia kilichomkuta mtu aliyevaa suruali yakubana?
Ripoti kutoka Australia inahusu ishu ya mwanamke mmoja kulazwa kwa muda wa kama siku nne hivi, kutokana na mishipa yake kupata majeraha baada ya kuvaa nguo ya kubana alafu akachuchumaa kwa muda mrefu hivi.
Mwanamke huyo  alijisikia kama ganzi hivi alipoinuka, akajaribu kutembea lakini hakufika mbali.. alianguka na baada ya muda kidogo alipata msaada wa kufikishwa Hospitali.
Dr. Thomas Kimber ni daktari katika Hospitali ya Royal Adelaide, Australia ambapo mwanamke huyo alipelekwa kutibiwa… Dokta anasema alishangazwa na jinsi ambavyo mgonjwa huyo alipata majeraha hayo yaliyotokana na nguo aliyoivaa.

No comments:

Post a Comment