Uyoga unazuia mtu kunenepa :Utafiti
Uyoga unatumika zaidi nchini Uchina Ulimwenguni kote kama dawa ya kupunguza unene.
Kwa
miaka uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya
kupunguza unene katika wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini
Taiwan.Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la mawasiliano ya mazingira unabaini kuwa madini ya Ganoderma Lucidum iliyoko ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.
Watafiti wanapendekeza kuwa uyoga hatimaye utatumika katika matibabu ya kupunguza uzito.
Wataalam wanasema kuwa sayansi hiyo ni nzuri, lakini kuweka maji yanayotokana na uyoga kwenye mikebe ya cola hakutawasaidia watu kupunguza uzito
G. lucidum imekuwa ikiuzwa tangu jadi kama kichocheo cha "kiafya na kurefusha maisha" hayo ni kwa mjibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Chang Gung.
Kwa habarim,matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment