Makamu wa rais Burundi atoroka
Moja kati ya makamu wa rais wa Burundi ametoroka nchini humo baada ya
kutangaza kuwa anapinga hatua ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza
kuwania muhula wa tatu.
Makamu huyo Gervais
Rufikiri amekimbia Ubljiji baada ya kuiambia runinga ya France24 kuwa muhula
huo wa tatu unakiuka sheria na katiba ya taifa hilo.Msemaji wa Serikali hata hivyo amekanusha madai hayo na kusema kuwa Rufikiri amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi.
Rufikiri amesema amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.
Msemaji huyo wa Serikali amesema iwapo Rufikiri ametoroka Burundi ni kwa maslahi yake mwenyewe wala hakuna yeyote aliyemtishia maisha yake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment