Sunday, June 28, 2015

FIDA LAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI WA TANGA KUANDIKA HABARI ZA WALEMAVU

 Mshauri wa miradi shirika la Fida International la Finland , Tero Mesiaisletho, akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya kuwajengea uwezo kuandika habari za watoto wenye ulemavu yaliyofanyika kituo cha (YDPC)  Tanga juzi.
 Waandishi wa habari  kutoka vyombo mbalimbali Mkoani Tanga, wakiwa katika mafunzo ya siku moja juu ya kujengewa uwezo kuhusu kuibua kero za walemavu Tanga yaliyoandaliwa na kituo cha kuwahudumia watoto walemavu (YDPC) na kudhaminiwa na shirika la Fida International la Finland   juzi.
 Mtaalamu wa lugha za alama kwa  watoto  ulemavu (viziwi) kutoka shirika la Fida International la  Finland, Virpi Mesiaisletho, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya siku moja ya  kuwajengea uwezo na kuandika habari za walemavu yaliyofanyika juzi Tanga.
 Waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali Mkoani Tanga, wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari za walemavu yaliyoandaliwa na kituo cha huduma kwa watoto wenye ulemavu (YDPC) na kufadhiliwa na  shirika la Fida Internationl la Finland juzi Tanga.

Mwandishi wa habari wa ITV, Mosess Fransiss, akitaka ufafanuzi  juu ya nafasi ya walemavu kupata taarifa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na kituo cha huduma kwa walemavu (YDPC) na kufadhiliwa na shirika la Fida International juzi.

No comments:

Post a Comment