Wednesday, June 24, 2015

NI KWELI SARAFU YA SHILINGI MIA TANO INA MADINI? MAJIBU HAYA HAPA

Ni kweli sarafu ya shilingi mia tano ina madini? Majibu yako kwenye hii video

Meneja BoT
Ilianza kama ishu ya kawaida hivi lakini muda ulivyozidi kwenda ikazidi kuchukua headlines kwenye mitandao ya kijamii kwamba eti kuna watu wananunua sarafu za shilingi mia tano za Tanzania alafu wanatumia madini ya sarafu hiyo kutengeneza vito kama mikufu hivi !
Sarafu Mia Tano
Nimepitia kwenye channel ya Youtube ya blogger mkubwa Tanzania,  na nimekutana na hii stori nikaona niisogeze hapa kushare na wewe pia.
Anayehojiwa ni Abdul M. Dollah ambaye ni Meneja Msaidizi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu TZ… Majibu yake ni haya kuhusu hiyo ishu; “Huu uvumi tumeusikia wananchi wengi wanakuja na kuulizia habari hiyo, huo ni uvumi tu na sio kweli kwamba kuna madini yoyote katika hii sarafu ya mia tano ambayo yanaweza kutengeneza vito vya thamani” >>> Abdul M. Dollah
Wakati tunaizindua hii sarafu mwaka jana tuliwaambia kwamba humu ndani kuna madini yya chuma kwa asilimia 94 na madini ya Nikel asilimia sita tu… Benki Kuu inaamini kwamba Wananchi wanadanganywa” >>> Abdul M. Dollah
coin
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog.

Jiunge na

No comments:

Post a Comment