Hii ni kali nyingine ya wanaume kutoka Japan, miaka 40 na hawajui wanawake!!
Tokyo ni moja kati ya miji maarufu inayofahamika kwa kua na huduma ya karibia kila hitaji la mwanadamu duniani, unaweza usiamini ila Tokyo iliopo Japan ni nchi inayo ongoza kwa kua na kila huduma inayokidhi mahitaji ya kimapenzi duniani kitu ambacho kinaweza kukufanya uione Japan kama ni walevi wa kufanya mapenzi. Lakini fikra hizi zinaweza zikabadilisha mtazamo wako kuhusu nchi hii pale utakapo kutana na Takashai Sakai mwanaume mwenye miaka 41 ambaye hajawahi kukutana na mwanamke toka azaliwe.
Akiwa katika miaka ya 40 na zaidi
mwanaume huyu hajawahi kabisa kukutana na mwanamke, kushikana mikono
wala kumkumbatia mwanamke yoyote. Lakini Takashai hayuko peke yake nchini Japan, kwani utafiti unaonyesha kwamba moja kati ya wanaume wanne wakijapan kwenye rika la miaka 30 hadi 40 hawajawahi katika maisha yao kua kwenye mahusiano ya kimapenzi, kushiriki tendo la ndoa wala kuoa!,
baadhi wakiwa wameanua kuishi maisha ya namna hio ila kwa wengi waliopo
hali hii haikua chaguo lao bali walijikuta tuu hawawezi, na wangependa
hali hii ibadilike kwani wanatamani kuonja ulimwengu huo sasa.
Lakini kwa asilimia kubwa ya wanaume wenye hali hii Japan darasa la uchoraji watu uchi “Nude Art Class”
ni suluhisho dogo kwa uhalisia walio nao na kwa upande wa pili ni fursa
pekee walionayo kumuona mwanamke akiwa mtupu!! Mmoja ya walimu wa
vipindi hivyo alisikika kwenye interview fupi akisema;
>>> “madarasa
kama haya hujaribu kuwasaidia watu kama hawa kuenjoy uumbaji wa jinsia
ya kike kupitia uchoraji, tunafanya hivi kuijenga saikolojia ya wanaume
hawa kuwaona wanawake sio watu wa kuwaogopa na hatimaye kuvunja uwoga
wao wa kufanya mapenzi, hii ndio dhamira yetu”.
Watafiti wamesema ongezeko la wanaume
wenye shida hii imekua ikionekana kama kikwazo kwa ukuwaji wa nchi
kwasabau idadi ya wanaume hawa inavyo ongezeka, idadi ya uzaaji
unapungua na hatimae kupunguza idadi ya watu nchini. Hili linaoneka kua
kama janga kwa moja ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment